Friday, 24 October 2014

SURVEY VETERANS YAILAZA MWANZA VETERANS 4-2 KATIKA ZIARA YAKE JIJINI MWANZA

Timu ya Survey Veterans kutoka Dar e salaam, imeilaza timu ya Mwanza StareheVeterans kwa magoli 4-2 katika uwanja wa CCM Kilumba Jijini Mwanza.Magoli ya Survey VeteransYalifungwa na Peter Ngasa, magoli 2,Innocent Lyimo na  Said Omary kwa mkwaju wa penati.Magoli ya wenyeji yalifungwa na Juma Amir Maftah na Mbuyi Yondani. Kikosi kilichoizamisha Mwanza Starehe Veterans kiliongozwa na Golikipa  Kilibe, fullbacks James Kabambo na Dr Rasul Ahmed, Center Backs Dr. Kibasa Na Kobi, Half Back six Mohamed Adam, Wingmidfielders Mzee Carlos na Shabani Kambabhe, Center forward Benson Hagai inside ten Peter Ngassa.
Kipindi cha pili yalifanyika mabadiliko, Mohamed Adam alitoka na Nafasi yake kuchukuliwa na Steven Nyenge, Benson Hagai  akaingia David Kiganga, Carlos akaingia Said Omary, Dr Rasul akaingia Ahmad, Kabambo akaingia Kisanga , akatoka Innocent akaingia Edward Lila. Hadi mwisho wa mchezo Survey Veterans 4 na wenyeji Mwanza Starehe veterans2.]

 kikosi kamili kilichoiangusha Mwanza Starehe Veterans kutoka kushoto walioinama mstari wa mbele Mohamed Adam (cap), Peter ngassa,Golikipa kilibe,james kabambo,Edward Lila, innocent lyimo, Osca Mwambungu, David kiganga. waliosimama mstari wa nyuma kutoka kulia ni Wilihem Ngasamiaku mwenye pensi ya jinsi, Steven nyenge (stevovo), Beki kisiki... Dr. D. Kibasa, Dr. Rasul Ahmed, Peter Mweta, Benson Hagai, Tonny Kiwale na  Carlos Mvula,


 mwal Bomba akitoa maelekezo baada ya mapumziko.... huku mzee carlos akiwa anapooza koo na maji baridi....
 ...Beki la kutumainiwa Dr D Kibasa akimsikiliza mwalimu kwa makini...

 M/kiti na katibu wakitoa shukrani kwa wachezaji baada ya game kwisha na kushinda goli 4-2
 ...Baadhi ya wanachama wa SVSC wakifuatilia maelezo ya m/kiti kwa makini...
 M/katibu Bw. Shabani Kambabheakiwa uwanja wa kirumba Mwanza kabla mchezo kuanza....

SURVEY VETERANS YATUA SALAMA UWANJA WA NDEGE WA MWANZA

BAADHI YA WACHEZAJI NA WANACHAMA WA svsc KATIKA PICHA YA PAMOJA UWANJA WA NDEGE WA MWANZA...

 .....Baadhi ya wachezaji wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mwanza....


 Katibu Mkuu wa survey Veterans na Mjumbe kamati ndogo ya Nidhamu wakiwa uwanja wa ndege wa Mwanza... baada ya kuwasili wakitokea Dar es salaam

KUNDI LA MWISHO LA SURVEY VETERANS LAPANDA NGEGE KUELEKEA MWANZA

AWAMU YA MWISHO YA WACHEZAJI NA WANACHAMA WA svsc WAMEONDOKA LEO SAA NNE MJINI DAR SALAAM KUELEKEA MWANZA KWA ZIARA YA KIMICHEZO




 Bw. Ngasamiaku akipata news katika sehemu ya kusubiri tayari kwa safari,......
 Mwenyekiti mstaafu Bw. Bakuza M.. pamoja na wanachama wengine katika waiting longe tayari kwa safari



 Stevovo", Cobi tayari kuelekea kwenye ndege







 M/kiti, Bw Kobi na M/M/kiti wakiwa angani kuelekea mwanza


 "Captain Ngasa na Mwl Bomba tayari kwa kupanda ndege





Thursday, 23 October 2014

BAADHI YA WACHEZAJI NA WANACHAMA WA SVSC WAWASILI UWANJA WA NDEGE MWANZA

 Carlos Mlinda namuona kwa mbali akiwa ameshika "begi lake la matairi" akiwa wa kwanza kuteremka kwenye ndege...
 M/Katibu naye akiwa ameshikilia begi lake kwa makini "kuogopa wezi"


Mhazini Msaidizi akifurahia jambo uwanja wa ndege wa Mwanza baada ya kuteremka .

TIMU YA SURVEY VETERANS ZIARANI MWANZA

TIMU YA SURVEY VETERANS IMEWASILI LEO ASUBUHI JIJINI MWANZA KWA ZIARA YA MICHEZO YA KIRAFIKI. TIMU MWENYEJI NI  MWANZA STAREHE VETERANS JIONI YA LEO  ITAKIPIGA NA TIMU YA.......

Juu na chini ni picha za Wachezaji na wanachama wa SVSC wakiwa uwanja wa ndege wa JNIA tayari kwa safari ya Mwanza na ndege ya Fastjet



 Baada ya Ku "Chech in" Katibu wa SVSC Bw. Suleiman Mgaya , Mjumbe kamati ndogo ya Nidhamu Bw. Frank Gaspar, Mhazini Msaidizi Bw. Benson Hagai na Golikipa namba moja wa SVSC wakisubiri muda wa kuondoka kuelekea Mwanza.


"Katibu mkuu na Bw. Frank walikuwa wakwanza kufika uwanjani"


"Tunazibua koki "

Bw innocent Lyimo, Captain Mohamed Adamu na Bw Benson Hagai wakiwa ndani ya Ngege
Picha ya chini inamuonesha M/Katibu Bw Shabani Kambabhe, Bw. Frank Gaspar na Bw. Suleimani wakiwa ndani ya ndege.......Safari njema....

Wednesday, 22 October 2014

LUGALO VETERAN YALAZIMISHA SARE NA SURVEY VETERANS

Timu ya Lugalo veterans ilipunguza uteja pale ilipolazimisha sare ya goli 2-2 na timu ngumu ya Survey Veterans mechi iliyochezwa katika uwanja wa nyumbani wa SVSC.Timu ya Survey Veterans imekuwa kinara kwa timu nyingi za veterans za mkoa wa dar esalaam na mikoanipia.

Angalia picha na matukio ya mechi hiyo...


Timu ya Lugalo veterans ambayo ilitoka sare ya magoli 2-2 na Timu ya Survey veterans.



ETINA BAR & RESTAURANT YANDAA PATI KWA AJILI YA KUWAPONGEZA SURVEY VETERANS

Mkurugenzi mtendaji wa Etina bar & Restaurant Bi Catherine Swai amewapongeza wapenzi na wachezaji wa timu ya Survey Veterans kwa ushindi wao walioupata katika Bonanza la Serengeti fiesta lililofanyika katika viwanja vya TCC Sigara Chang'ombe. Pia Mwenyekiti wa SVSC Bw. Peter Mweta alimshukuru kwa kutambua mchango wao katika kulitangaza jina la Bar hiyo. 
Mwenyekiti Bw. Peter Mweta aliwaongoza wachezaji na wanachama katika zoezi la kukata keki kama matukio ya picha yanavyoonesha....

" KEKI YA USHINDI"






 Mkurugenzi wa Etina Bar & Restaurant Bi Catherine Swai akiwa katika picha ya pamoja na Kipa mkongwe Bw. Peter Poka, Bw. Innocent na Bw, Musa Siwiti katika sherehe hiyo....



" Hii mishkat kiwango" Bw. Omar bawaziri akifurahia mshikaki huku Bw. Kilibe naye akijilamba kwa utamu.....


 Bw. akifungua Champagne kuashiria ufunguzi wa sherehe hiyo...

" Isee tamu" mwasenga anawaambia wanachama na wapenzi wa SVSC



 Bw. Omar Bawazil na Bw. Joseph Mwasenga wakiteta jambo siku ya sherehe

" Kukata keki raha" Hivyo ndivyo inavyoeleka kusema  Mwenyekiti Bw. Peter Mweta akikata keki nyuma yake Captain Bw. Peter Ngasa, Bw. Steven Nyenge ,Blogger Bw Musa Siwiti na Mjumbe kamati ya ufundi Bw. Ally Mgaya wakishuhudia kwa karibu kabisa.
 Sherehe iliambata na kinywaji kama ambavyo Mwl Bw. Ramadhani Bomba akipata mvinyo akishereekea ushindi