Saturday, 9 August 2014

SVSC YALAZIMISHWA SARE NA KIKOSI B CHA TIMU YA COASTAL UNION YA JIJINI TANGA

Timu ya SVSC katika mechi yake ya pili jijini Tanga ililazimishwa sare na Mabingwa wa Uhai Cup kikosi cha pili cha Wagosi wa Kaya Costal Union katika uwanja wa Mkwakwani baada ya  kutoka sare ya bao 1-1 baada ya kuongoza kwa dk 70 za mchezo bao lililowekwa kimiani na mshambuliaji hatari Moses katika dak ya 27 kipindi cha kwanza. Dk 20 kabla mpira kumalizika vijana wa Costal union walisawazisha baada ya kutokea piga nikupige langoni mwa survey vetens.

PICHA MATUKIO YA MCHEZO HUO


Juu na chini ni kikosi kilichotoka sare na Mabingwa wa Uhai cup Timu B ya Costal Union 



 Picha chini Inamuonesha Capt Mohamed Adam "Zengwe" akionesha maufundi katika uwanja wa mkwakwani mjini tanga kabla mechi kuanza

 Picha juu kikosi cha Survey kikipasha misuli moto kwa ajili ya maandalizi ya mchezo....

Benchi la ufundi likiongozwa na Mwl Ramadhani Bomba likifuatilia mchezo kwa makini.....

TIMU YA SURVEY VETERANS YAIBUGIZA MAGOLI 2-1 TIMU YA TANGA VETERANS

Timu ya SVSC imeanza vizuri ziara yake jijini Tanga kwa
kuifunga timu ya Kombaini ya jijini Humo kwa magoli 2-1 Magoli yakifungwa na washambuliaji hatari wa pembeni David Kiganga na Salvatory Malongo. Huku goli la kujifunga la Beki nguli wa pembeni likiwapatia Kombaini ya Tanga goli la kufutia machozi.


 Muuaji wa goli la kuongoza. David Kiganga akiwa amepumzika baada ya kipindi cha kwanza kumalizika

Picha chini unamuonesha muuaji wa goli la pili Sarvator Malongo ikitoka uwanjani baada ya kumaliza kazi yake.

 Picha juu inamuonesha Said Mahoka akiwachua viungo wachezaji wakati wa mapumziko..
 Captain Ahmad wakati wa mapumziko
 ....Wanaume tumemaliza kazi.... Ndivyo capt Ahmad akiwaambia wenzake Osca na Carlos baada ya mchezo kumalizika.



Friday, 8 August 2014

TIMU YA SURVEY VETERANS ZIARANI JIJINI TANGA.

Timu ya SVSC ikiwa katika kituo cha mabasi yaendayo Mikoani na nchi jirani tayari kwa safari ya kuelekea Tanga pamoja na wadhamini wao National social security fund (NSSF)

Katibu Mkuu wa SVSC Bw. Suleiman Mgaya na Makamu Mwenyekiti nao walikuwa miongoni mwa wachezaji walioongozana na timu hiyo


Juu na chini ni wachezaji wa SVSC wakiwa kituo cha mabasi yaendayo mikoani tayari kwa safari


Timu ikiwa ndani ya Bus la Ratco Kuelekea Tanga

Picha za hapo chini zinaonesha Timu imewasili Tanga salama 

Timu imewasili salama jijini Tanga



Picha juu na chini inawaonesha wadhamini wakuu wa SVSC  (NSSF) wakiwa katika sare ya pamoja na wachezaji baada ya kuwasili salama jijini Tanga.




Wednesday, 6 August 2014

Kikosi kilichoiangamiza Kibangu Veterans


Picha ya pamoja na wachezaji wa kibangu kabla ya mechi ambayo walilala kwa bao 1-0

Tuesday, 5 August 2014

Timu imeanza zamani kipindi hicho katibu anavaa sosksi ndefu! hahahahahaha... Hebu jaribu kuwatambua hao wachezaji.......

Monday, 4 August 2014

Ndugu wana michezo, ni mwendelezo wa matukio ya kumuaga ndugu yetu Bw. Bruce Heilman ambaye anamaliza muda wake wa kukaa Tanzania. Picha zifuatazo zinaonesha matukio.
Picha chini... inamuonesha Mwenyekiti wa SVSC Bw. Peter Mweta akimkabidhi Bw. Bruce Heilman kikombe chenye nembo ya timu ya SVSC kama mojawapo ya zawadi huku Katibu mkuu Bw. Suleiman akishuhudia kwa karibu.











M/M/kiti Bw. Rasul Ahmed alimkabidhi Bw. Bruce Helmain Kinyago chenye nembo ya timu ya SVSC kama moja ya zawadi alizokabidhiwa...





Mwenyekiti akionesha kikombe chenye nembo ya timu kikiwa kimeandaliwa na uongozi wa SVSC kama mradi wa kutunisha mfuko wa timu. Vikombe vipo kwa mwanachama na wapenzi watakao hitaji. Gharama yake ni tsh. 18,000/= tu.

 Matukio yaliendelea kwa wanachama na wapenzi kupata chakula cha pamoja  kwenye makao makuu ya club Etina Bar & Restaurant. Bw. Mbwete na Bw. Kabambo wakipata chakula.....

Hafla ya kumuaga ndugu yetu Bruce

 ....Hiki chakula ni kitamuu!!!!! Bw. B Magadula akimweleza Joseph wakati wakipata msosi


 ...".Ongeza ongeza.... hii biriani tamu sana"

Mwisho Bw. Bruce aliwashukuru wanachama na wachezaji wenzake ( hawapo pichani) kwa moyo wao wa upendo. na kuwatakia maisha mema na yenye furaha. Mungu akupenda tutaonana tena alimalizia.....