Saturday, 2 January 2016

MATUKIO YA PICHA KATIKA SHEREHE YA KUUAGA MWAKA 2015 NA KUUKARIBISHA MWAKA 2016




Innocent Lyimo na Frank G mwenye Kibagalashia wakipata chakula katika sherehe hiyo

Mwenyekiti kulia na Aaron Nyanda wakipata chakula


Dominic Mbwete na wanawe wakipata msosi



Captain Ahmad pamoja na wanachama wengine wakipata msosi

Katibu mkuu Suleiman Mgaya na watoto wake wakipata chakula

Captain Mohamed Zengwe na Bakuza wakiwa katika foleni ya chakula




Bunyabunya Shamakala akigawa chakula


Benson Mwemezi akipakua chakula

wadau wakipata chakula

"Kula mwanangu" Katibu akimpa mtoto wake chakula katika sherehe hiyo

"Blogger kazini" Pia akipata msosi katika sherehe hiyo

Musa Siwiti, Benson Hagai katikati na Mohamed Zengwe wakipata msosi





















MATUKIO YA PICHA KABLA YA SHEREHE KUUKARIBISHA MWAKA MPYA 2016

REFA (Bunyabunya) aliyechezesha mechi kati ya Timu Sule na Timu Shebby

Baadhi ya wachezaji wa Timu Shabani wakijiandaa kabla ya mchezo









KATIKA KUELEKEA SHEREHE ZA MWAKA MPYA. TIMU SULEMANI YAIFUNGA TIMU SHABANI GOLI 3-1


Timu Shabani kabla ya mchezo kuanza
Survey veterans katika kuukaribisha mwaka mpya 2016. walicheza mechi ya kirafiki kati yao ambapo Mwalimu alipanga timu mbili ambazo ziliitwa. "Team Sulemani" na "Team Shabani. " ambao Bw. Sulemani ni Katibu Mkuu wa SVSC na Bw. Shabani ni Kaimu Katibu.Mchezo ulianza kwa kila timu kujilinda na kucheza kwa taadhari. Ilikuwa timu Sulemani iliyoanza kupata goli kupitia mshambuliji wao Aaron Nyanda baada ya kupata pasi akiwa katika eneo la kuotea na mabeki wa timu Shabani kumuacha wakizani ameotea. Baada ya muda baadae timu Sulemani walipata goli la pili kupitia kiungo wao hatari Abdala Kassimu.

Hadi timu zinaenda mapumziko magoli yalikuwa 2-0. Kipindi cha pili kilianza kwa kila timu ikiwa imefanya mabadiliko. iliwachukua muda mfupi kupata goli kwa njia ya penati lililofungwa na Moses baada ya beki wa Timu Sulemani kumchezea rafu kwenye eneo la hatari.

Dakika 20 kabla mpira kumalizika Timu Sulemani iliongeza goli la tatu kupitia mshambuluaji wao Moses. Hadi mpira unaisha timu Suleimani walishinda goli 3-1.

Katika mchezo huo refa alichangia kwa kiasi kikubwa kwa timu Shabani kufungwa baada ya kuonesha upendeleo wa wazi kabisa. Na hata timu Sulemani ilipopata goli la pili alionekana kushangilia kisirisiri. Hii inashauriwa wakati mwingine achaguliwe refa ambaye hana upande katika timu zinazopambana.
Timu Sulemsni kabla ya mchezo kuanza.

SALAMAU ZA KRISMAS NA MWAKA MPYA KUTOKA MWENYEKITI WA SURVEY VETERANS

Wanachama na wapenzi wa SVSC napenda niwatakie heri ya Krismasi na mwaka mpya ninyi na familia zenu. Matukio mengi yametokea aktikati yetu mazuri na mabaya sina haja ya kuyataja lakini Mungu ni mwema ametufikisha hapa.

2015 imeisha Kwa Amani,Upendo ,mshikamano na ushirikiano wa hali ya juu sana ndani ya SVSC naomba tuhamie navyo 2016,changamoto kubwa tuliyopata ni kipato cha kuendesha timu yetu Kwa niaba ya uongozi nawashukuru sana Kwa kutuwezesha kuimudu Ila bado haijaisha tumehama nayo mwaka huu 2016,Napenda kutumia maneno yaliyotumiwa sana na hayati mwl Nyerere akimnukuu aliyekuwa rais wa marekani Kennedy,"jiulize kwanza utaifanyia nn Svsc sio Svsc itakufanyia nn wewe". Mungu ibariki Svsc. Karibuni mazoezini.
Peter Mweta,
Mwenyekiti