Friday, 28 September 2018

SHEREHE YA MCHEZO YA SVSC vs BBV ILIISHIA HIVI.......

Baada ya mchezo kumalizika katika uwanja wa BBV sherehe iliendelea katika ukumbi wa Maendeleo Bar wanaoonekana kwenye picha ni wachezaji mchanganyiko wageni na wenyeji.

Supu ililiwa kama kawaida pamoja na vinywaji laini.....

Kama kawaida vinywaji vigumu vilikwepo na wachezaji waliendelea kufurahi kwa pamoja....

David Kiganga kushoto na Idd Ngaoneka wakiendelea na supu huku viburudisho vikionekana kwa mbalaaaali...vikileta maji ya kunawa na kuondoa mabakuri hahahahahahah!!!!


KUELEKEA MCHEZO WA SVSC vs BBV

Kabla ya mchezo kuanza timu ilianza kufanya mazoezi madogo madogo katika uwanja wa Boko Veterans. kutoka kulia ni Suleiman Mgaya, David Kiganga, James Kabambo, Golikipa na John Mbitu wakipasha misuri moto kabla ya mchezo kuanza.

Kundi lingine likifanya mazoezi kutoka kushoto ni James Kabambo, Salum Mvule, Dkt Mwinyi Omary,Dkt Mbunda na Beki hatari Peter ndossa

Peter ndosa kushoto, Bruce Helman katikati na Michael wakipasha misuri kabla ya mchezo kuanza.

Kaptain msaidizi Hamad Shaweji akiondoza wachezaji wa SVSC hawapo pichani kujiandaa na mchezo.

John Mbitu mbele, David Kiganga nyuma na James Kabambo wakimsikiliza muongoza mazoezi hayupo pichani kujiandaa na mchezo.


Farnk Gaspar, Suleiman Mgaya, Kabambo jr na wengine katika kuweka miili yao sawa kabla ya mchezo kuanza.















Musa Siwiti (Blogger wa Timu akipasha misuri kabla ya mchezo kuanza.

















Thursday, 27 September 2018

BOKO BEACH VETERANS YABANWA NA SURVEY VETERANS


Timu ya BBV ilijikuta katika wakati mgumu pale ilipolazimishwa sare ya magoli 3-3 na timu Kisiki ya veterans mkoa wa Daresalaam na nchi nzima kwa ujumla. BBV ikiwa mbele kwa magoli 2 hadi kipindi cha pili ilijikuta katika wakati mgumu pale Benson Mwemezi akipokea pasi murua kutoka kwa Dr. Shukia alipoandikisha bao la kwanza kabla ya Iddy ngaoneka na Hasan Mussa kukamilisha sherehe hiyo.

Timu ya BBV katika ukaguzi kabla ya mchezo kuanza. Captain wa SVSC Peter Ngassa kushoto kwa Mwenye kitambi kikubwa alichezea timu ya BBV.

Wachezaji wa timu ya SVSC wakisalimiana na wachezaji wa BBV kabla ya mchezo kuanza.

Mwl Ramadhani Bomba akisalimiana na wachezaji wa BBV kabla ya mchezo kuanza.

Kaptain wa SVSC akisalimiana na waamuzi huku kaptain wa Timu ya BBV akiangalia kwa makini.

Captain wa mchezo Carlos Salum wakijadiliana na waamuzi kabla ya mchezo kuanza

Mwl Bomba mwenye Jezi ya Manchester akifuatilia mchezo kwa makini

Benchi la Timu ya SVSC wakiwa makini kufuatilia mchezo.