Sunday, 17 December 2017

INNOCENT LYIMO: BINGWA WA MBIO ZA MITA 100 BONANZA LA NEIGHBOURS

Innocent Lyimo akipokea zawadi yake ya ushindi wa mbio za mita 100 kutoka kwa mchezaji mwenzake John mbitu katika bonanza la ujirani mwema

ALBERT KAJALA SENGO MFUNGAJI BORA WA MASHINDANO YA BONANZA

Albert Sengo mfungaji bora wa bonanza akiwa na watoto waliokuja kushangilia na kufuatilia michezo hiyo

MATUKIO YA PICHA KATIKA BONANZA HILO

Hamis Gaga (Gagarino) akipokea zawadi yake ya uchezaji bora wa mechi ya kwanza





















SURVEY VETERANS MABINGWA BONANZA LA NEIGHBOURS


Timu  hatari ya SVSC iliweza kutwaa ubingwa wa Bonanza siku ya jumamosi katika uwanja wa Neighbour's Madale Mivumoni kwa kuzifunga timu zote zilizoshiriki bonanza hilo. Mechi ya kwanza SVSC ilicheza na Madale Veterans na kuwafunga magoli 4-2,huku magoli mawili yakifungwa na Albert Sengo, Hamis Gaga (gagarino) akifunga goli moja na goli la nne likifungwa na Benjamin Magadula.

Mechi ya pili tulicheza na Wenyeji Neighbours Veterans na kuwafunga goli moja liliwekwa kimiani na Chacha Kibago. Mechi ya tatu SVSC ilishinda kwa magoli mawili magoli yote yakifungwa na  Albert Sengo kwa kumalizia shuti kali la Musa Siwiti ambalo golikipa alilitema.

Mchezo kwa ujumla ulikuwa mzuri na timu ilicheza kwa uwelewano mkubwa sana. Pia timu ya SVSC ilitoa washindi wawili kwenye mbio za mita 100. Innocent Lyimo akichukua zawadi ya Ushindi wa kwanza na Joseph Mwasenga akichukua ushindi wa tatu.
Innocent Lyimo aliyevua shati akipokea zawadi yake ya mshindi wa kwanza wa mbio za mita 100 baada ya kuibuka mshindi kati ya washiriki 8 walioshiriki mbio hizo

Pia Golikipa namba moja Sha_Pelle alichukua golikipa bora wa mechi ya kwanza na Hamisi Gaga alichukua uchezaji bora mechi ya kwanza
Golikipa bora wa bonanza  Sha_pelle akiwa hoi bada ya kumaliza mchezo wa kwanza na kuchaguliwa kuwa golikipa bora wa mashindano. Pia ni golikipa aliyefungwa goli moja tu katika michezo yote mitatu aliyocheza.