Friday, 29 December 2017

MWALIMU BOMBA KATIKA KAZI YAKE YA KILA SIKU


Mwalimu Ramadhani Bomba amekuwa ni mtu wa pekee katika timu ya SVSC. Ni mwalimu wa nidhamu, mwalimu wa mpira na mambo mengine yanayohusu maisha binafsi. Hii ni pale ambapo mchezaji anapoenda kinyume anamrekebisha kwa kumuonya na kumfanya awe mchezaji mzuri. Baada ya Peter Simon kukengeuka Mwalimu pamoja na wanamichezo wengine walimtaka kujirekebisha na kwenda sawa na falsafa ya Survey Veterans ya Upendo, uvumilivu, kuheshimiana kati ya mtu na mtu uwanjani na nje ya uwanja. Tunampongeza sana Mwalimu Bomba

SURVEY VETERANS GET TOGETHER PARTY YAFANA


Ilikuwa siku muhimu sana kwa wana Survey wote, Wapenzi, wanamichezo na wanachama kwa ujumla pale ambapo walikusanyika kwa pamoja kwa ajili ya kusherehekea siku kuu ya krismas. Ni utaratibu ambao wamejiwekea kila panapokuwa na sikukuu kubwa kama Pasaka, krimas na Idd.

Tuesday, 26 December 2017

NSSF YALAZIMISHA SARE NA SURVEY VETERANS


Timu ya NSSF ililazimisha sare ya magoli 2-2 na timu ngumu ya SVSC. Timu hii ya NSSF imekuwa mpinzani mkubwa sana kwa SVSC kwa mwaka huu maana tumekutana mara tatu na mara zote tumetoka sare.




Captain Peter Ngasa Mwenye notebook mkononi akitoa maelekezo kwa wachezaji kabla ya mchezo kuanza. aliyekaa chini ni Chacha kibago