Sunday, 30 August 2015

ZAWADI YA TIMU KWA RAMADHANI BOMBA


Timu ya SVSC katika kufahamu umuhimu wa Mwl, kwa kushirikiana na Mwl Bomba walikubaliana tumnunulie king'amuzi cha Azam kama zawadi ya timu kwake,
Matukio ya picha hapo chini yanaonesha mahabidhiano hayo.
M/M/kiti Dkt. Rasul akikabidhi king'amuzi kwa Mwl Bomba kama zawadi ya timu katika siku Bomba Day huku Capt Mohamed Adam akishuhudia kwa karibu.


Bw, Ramadhani Bomba akiangalia kwa furaha zawadi yake 







SHEREHE YA KUADHIMISHA BOMBA DAY ETINA BAR & RESTAURANT

Baada ya mchezo wa kuadhimisha siku hii muhimu, kulikuwa na sherehe iliyoandaliwa na wanachama kwa ajili ya kumpongeza mwalimu kwa kazi kubwa anayoendelea kuifanya katika timu. MATUKIO YA PICHA ANAONESHA,
Katibu Mkuu Suleiman Mgaya , Kaimu Katibu Shabani K. aliyeshika simu na Kaimu Mwenyekiti Dkt, Rasul wakiwakaribisha wapenzi na wanachama katika sherehe ya kuadhimisha siku ya Bomba day Etina Bar &Restaurant.

David Kiganga akifungua champagn kuashiria kuanza kwa sherehe hiyo.

Peter Ngassa (Capt) kushoto,John MBitu  katikati na Misheki  kulia wakifuatilia kwa makini malezo ya Katibu.

....Kaimu Mhazini Benson Mwemezi kulia na Capt Adam Zengwe wakisikiliza hotuba ya Katibu ....

Ramadhani Bomba kushoto akitoa neno la shukrani kwa wapenzi na wanachama wa SVSC hawapo pichani katika siku ya kuadhimisha siku ya Bomba Day huku  M/M/kiti Dkt Rasul akifuatilia kwa makini.

Ikafika muda wa msosi kama ambayo katibu Suleiman Mgaya , Joseph Mwasenga wanagonga Menu.


John Mbitu, Hgai, Misheki na wengine wakiwa wanapata Menu

Ramadhan Bomba ambaye ilikuwa siku yake muhimu akipata msosi

Dkt Rasul akipata msosi siku ya Bomba Day


.....KIMEISHA......

Blogger  Musa Siwiti alikuwa Kazini kuhakikisha Mambo yote yanarekodiwa kwa usahihi na kuingizwa katika blog ya Timu...



Blogger wa Timu Musa Siwiti kushoto, Ahmad Shaweji katikati na Mahoka wakiwa wanapata Msosi katika siku ya Bomba day


MATUKIO YA PICHA KATIKA MCHEZO WA KUMUENZI MWL RAMADHANI BOMBA

MATUKIO YA PICHA KATIKA MCHEZO WA KUMUENZI MWL RAMADHANI BOMBA
Musa Siwiti kushoto, Beki hatari Joseph Mwasenga katikati na James Kabambo kulia kabla ya mchezo

(jezi imempendeza sana hii) Frank Gaspa  timu Zengwe 

Beki kisiki Makoye Timu Zengwe

Luku akionesha alama ya vidole viwili kwamba tutawafunga 2 ila Zengwe la Muddy Zengwe lilisababisha tufungwe tatu

Hii ndiyo Timu ZENGWE iliyoibuka na Ushindi siku ya Bomba Daya kutoka kulia waliochuchumaa ni Makoye,Luku,Ramadhani,Gaga,Hassan,Suleiman na waliosimama kutoka kushoto ni Kiganga,Van Bomel,Ally,Innocent,Ahmed,Frank,Shaban,Carlos, Zengwe na alifa.

BOMBA DAY, BOMBA DAY, BOMBA DAY

Siku hii muhimu kwa wana SVSC ni siku ya kukumbukwa sana kwani timu ilizindua pia jezi mpya kwa ajili ya timu kama picha zinavyoonesha.
Jezi mpya kama zinavyooneka na . Hii ni Timu Bomba ndiyo waliopata nafasi ya kuzindua jezi hizi.Kutoka kulia walioinama ni Mbunda,Osca,Noel,Kabambo,Musa,Feyi,Mwasenga na waliosimama kutoka kushoto ni Charles, John Mbitu,Mahoka,Kione,Ally,Rasul,Juma,Bomba,Hagai na Mzee wa timu NDunguru.

BOMBA DAY ,BOMBA DAY, BOMBA DAY, BOMBA DAY, BOMBA DAY, BOMBA DAY

BOMBA DAY ,BOMBA DAY, BOMBA DAY, BOMBA DAY, 

Hivi ndivyo ilikuwa ikitamkika baada ya wazo zuri lililotolewa na mmoja wa wanachama wa SVSC katika kutambua umuhimu na utayari wa kuitumikia timu ambao Bw, Ramadhani Bomba ameuonesha katika kuitumikia timu toka imeanzishwa kama mwl wa timu,
Wazo lilitimia pale wanachama kwa pamoja waliamua kutoa michango yao ili kufanikisha shughuli hii. Tarehe 29/08/2015 ilikuwa siku muhimu katika Timu ya SVSC  baada ya kuadhimisha siku hii pale ambapo Mwalimu Bomba kwa Kushirikiana na Capt Mohmed Adam (Zengwe) walipochagua timu miongoni mwa wanachama wa SVSC ambapo Timu y mwalimu iliitwa (Team Bomba) na Timu nyingine iliitwa (Team Zengwe).
Wachezaji wa Timu Bomba walikuwa kama wafuatao...

  1. Noel (kipa)
  2. Joseph Mwasenga
  3. Rasul Ahmed (Dkt)
  4. James Kabambo
  5. Osca Mwambungu
  6. Charles Antipass
  7. Hagai Benson
  8. Mahoka Said
  9. Athuman Kione
  10. Bilauli
  11. Juma Massawe
  12. Ally Mgaya
  13. Mbunda Richard
  14. Musa Siwiti
  15. Sengo Arbat
  16. Idd Ngaoneka
  17. Ally Mgaya
  18. Alfa
  19. Edwin
  20. Ngassa Peter
  21. John MBitu
  22. Moses
  23. Feyi


na Timu Zengwe wachezaji waliochaguliwa walikuwa kama wafuatao,
  1. Ramadhani Njuma (kipa)
  2. Said
  3. Hemed Salum
  4. Mohamed Adam
  5. Van Bomel
  6. Gaga Hamisi
  7. Frank Gaspar
  8. Hassan Hassan
  9. Mzee Halifa
  10. Suleiman  Mgaya
  11. Carlos Mlinda
  12. Innocent
  13. Shabani K
  14. Maulasa
  15. Kipese Peter
  16. Luku
Mchezo ulianza kila timu ikicheza kwa taadhari lakini hadi mapumziko timu zote mbili hazikufungana. Kipindi cha pili kilianza kwa kila timu kushambulia kwa zamu, Ilikuwa Timu Bomba iliyoanza kupata goli kupitia kwa Moses na baadae Sengo Arbart aliongeza la pili. Timu Zengwe, walianza Zengwe kwa kufanya mabadiliko. 
Iliwachukua dakika 10 kupata goli la kwanza kupitia kwa Innocent Lyimo aliyemalizia mpira uliotemwa na golikipa. Alikuwa Innocent Lyimo tena aliye ipatiagoli la kuongoza Timu ya Zengwe baada ya kuupiga mpira golini huku golikipa akiwa hayupo. Hadi mwisho wa Mchezo Timu Zengwe ilishinda kwa magoli 3-2.