Sunday, 19 July 2015

KATIKA KUSHEREHEKEA SIKUKUU YA EID PILI, BW, SHABANI K. ALIZALIWA

Tarehe 19/07/.... alizaliwa M/katibu wa Survey Veterans  Bw. Shaban K. katika siku ya sikukuu ya Eid pili ambapo M/kiti wa SVSC Bw, Peter Mweta aliungana na wanachama na wapenzi wa Survey Veterans katika kumpongeza Bw,Shabani katika siku yake ya kuzaliwa na kumtakia maisha marefu yenye amani na furaha tele.

 Pia M/kiti alifungua shampagn isiyo na kilevi katika kumpongeza Bw, Shabani K. kwa kuzaliwa leo.
Matukio ya picha yanaonesha mfululizo wa tukio hilo

Picha juu na chini zinamuonesha M/kiti Bw. Peter Mweta akifungua champaign kwa ajili ya kumtakia heri K/Katibu Bwa Shabani Selemen Kambabhe mwenye kofia  katika siku yake ya kuzaliwa. Macocha Tembele akiangalia kwa karibu



K/katibu Bw, Shabani S. Kambabhe akitoa shukrani kwa wanachama na wapenzi wa SVSC ambao walijumuika  pamoja katika kufanikisha sherehe ya Eid pili na kumtakia heri katika siku yake ya kuzaliwa Huku mjumbe kamati ya nidhamu Bw, Frank Gaspar akisikiliza kwa makini..
M/kiti na katibu wakiteta jambo katika sherehe hiyo..

 M/kiti Bw, Peter Mweta mwenye jezi nyeupe waliosimama , Katibu mkuu Bw, Suleiman Mgaya mwenye T- shirt nyeusi, Bwa, Frank Gaspar mwenye T- shirt ya pundamilia , M/M/kiti Dkt Rasul mwenye miwani aliyekaa ,Mzee Harifa mwenye shati la dukani, wakimsikiliza K/Katibu Bw, Shabani katika sherehe hiyo.....



PICHA ZOTE KWA HISANI YA BLOGGER



SURVEY VETERANS YAMPONGEZA MWANACHAMA WAO Dkt NGASAMIAKU KWA KUPATA Phd

M/kiti wa Survey Veterans Bw Peter Mweta aliungana na wanachama wa SVSC kumpongeza Dkt Ngasamiaku kwa kumaliza masomo yake na kupata Phd yake.
Dkt Ngasamiaku ,alipopewa nafasi ya kusema chochote alisema', "Nawashukuru sana wapenzi na wanamichezo wa SVSC kwa maombi yenu ambayo naamini kwa njia moja ama nyingine yalifanikisha mimi kufikia hatua hii kubwa ya kielimu Mungu awabariki sana". Mwanachana na mchezaji wa SVSC Bw. Innocent Lyimo alifungua Champaign kuashiria furaha na upendo katika tukio hili.
M/kiti kwa mara nyingine alimpongeza Dkt Ngasamiaku kwa hatua hiyo kubwa kielimu na kuwashukuru wanachama kwa umoja wao na mshikamano.

Matukio ya picha hapo chini yanakamilisha tukio hilo muhimu
 ..Hongera sana Dkt Ngasamiaku...M/kiti wa SVSC  Bw. peter Mweta akimpongeza Dkt Ngasamiaku kwa hatua aliyoifikia kielimu.

 "..Napenda nichukue fulsa hii kuwashukuru sana wanachama wenzangu kwa upendo wenu. Mungu awabariki sana." Hayo ni maneno aliyoyatoa Dkt Ngasamiaku katika sherehe ya kumpongeza baada ya kumaliza masomo yake na kupata Phd.
 Bw. Innocent lyimo alifungua Champaign kayika kuhitimisha sherehe hiyo.

SURVEY VETERANS YASHEREHEKEA EID PILI KWA FURAHA

Kama ilivyo ada, kwa timu hii, kila mwaka husherekea kwa pamoja siku kuu ya Eid pili kwa matukio mbali mbali ikiwa ni njia mojawapo ya kukutana pamoja, kula pamoja na kufurahi pamoja.

Sherehe ya mwaka huu inaweza ikawa imevunja rekodi kati ya sherehe kama hii zilizopita maana ilikuwa inaandaliwa kwa umakini na ueledi mkubwa chini ya Mhazini Mkuu Dkt R. Shukia (Sha-Makala). Wanachama pia walikuwa wengi ukilinganisha na miakailiyopita penhine kutokana na kuhamasishwa mara kwa mara katika kuhakikisha sherehe hii inafanikiwa
.
Picha za matukio ya shsrehe hii hapo chini zinaonesha furaha jinsi ilivyokuwa.
M/kiti Bw Peter Mweta , M/Mkiti Dkt Rasul wakiwaongoza wanachama wa Survey Veterans katika kachula cha mchana katika kuadhimisha sikukuu ya Eid pili katika ukumbi wa Etina Bar & Restaurant

M/Mkiti Dkt Rasul mbele , Macocha  na Mbwete wakiwa katika kupakua chakula katika hafla iliyoandaliwa na wanachama na wapenzi wa Survey Veterans katika ukumbi wa Etina Bar & Restaurant siku ya Eid pili