Thursday, 5 April 2018

SALAMU ZA PASAKA KUTOKA MWENYEKITI WA SURVEY VETERANS SPORTS CLUB


Wadau habari za Jioni, wageni wetu kutoka Zanzibar waliondoka jana na kufika salama Unguja.
Napenda kutoa shukurani za dhati kwenu nyote mlioshiriki na hata wale ambao hawajashiriki najua mlikuwa na nia ila mambo yaliingiliana.
Kwa niaba ya kamati ya utendaji na ya wageni nasema ASANTENI SANA.
Shukrani ziende kwa wale wote waliopewa majukumu na kuyatekeleza kikamilifu kabisa, Katibu, Mhazini,wapokeaji michango Mwalimu Bomba na Babu Carlos (wajela jela) 🤩, Mchaga Frank, Ali Mgaya,Shabani katibu Msaidizi,Mchaga Inno, Oliver Katanje(Dr) na Jumuiya yote ya SVSC.
Vile vile Shukrani ziende kwa baadhi ya Etina Members waliolisikia na kutuchangia, Mhazini alilipia full Chai ya siku ya kwanza kwa wageni na Kurugenzi ya Etina ilituchangia full chai ya mwisho kwa wageni. 🙏🏾🙏🏾🙏🏾
Mwisho niwakumbushe tu kuwa ile ni michango ya kila mwezi ambayo tunatakiwa tuwe tunachanga ,Mhazini atatoa jedwali ili tuendelee kutoa. Niwatakie jioni njema.
M’kiti

Tuesday, 3 April 2018

SURVEY VETERANS BINGWA WA HISTORIA MICHUANO YA PASAKA 2018

Captain wa timu ya SVSC Peter ngassa akinyanyua juu kombe la ubingwa wa Michuano ya Pasaka kwa mwaka 2018 baada ya kukabidhiwa na mgeni rasmi Mkurugenzi wa Ufundi TFF Mwl Salim Madadi aliyemwakilisha Naibu katibu mkuu wa TFF Bw. Wilfred Kidau. Pembeni ni Mwenyekiti wa SVSC Bw. Peter Mweta akishangilia kwa furaha.
Mgeni Rasmi Mkurugenzi wa Ufundi TFF Bw. Salim Madadi akitoa maelezo mafupi kwenye ufungaji wa mashindano ya Pasaka kabla ya kutoa zawadi na kukabidhi kikombe kwa washindi

Mwenyekiti SVSC Bw. Peter Mweta akiwa ameshikiria kombe la ubingwa kabla ya hafla ya kukabidhi kombe. Kushoto ni mwenyekiti wa Wazee Sports  Bw. Giga akiwa anasikitika baada ya kukipoteza kikombe hiki kwa mihula mitatumfurulizo
...Haikuwa Rahisi/......Mfungaji wa goli la ushindi Albart Sengo aliumia baada ya kusukumwa na beki wa wazee sports na kuumia goti. Pole sana kwake //,,,

....Haikuwa raihisi tulipambana kupata ubingwa huu.." Blogger"





wachezaji wa timu SVSC wakimsikiliza mgeni rasmi baada ya mchezo kumalizika


...Ushindi Raha//...

Steven Nyenge "Stevovo" akifurahia jambo na mgeni rasmi Mwl Madadiwakati wa utoaji wa mkono wa pongezi kwa kunyakua ubingwa mara tatu mfurulizo






...Benteke  John Mbittu akisalimiana na  mgeni rasmi kipindi cha kutoamkono wa pongezi  kwa kunyakua  ubingwa kwa mara tatu mfurulizo


Mbunge wa Chalinze Bw. Ridhiwani kikwete akisalimiana na Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF Mwl Salimu Madadi ambaye alimwakilisha Naibu katibu mkuu Bw. Wilfread Kidau katika uwanja wa Taifa.

Kaptain Peter Ngasa akikabidhiwa kikombe cha ubingwa na Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF Mwl Salimu Madadi ambaye alimwakilisha Naibu katibu mkuu Bw. Wilfread Kidau katika uwanja wa Taifa.

.....Hongera kwa kuzaliwa.. Maneno ya Innocent Lyimo "Mchaga" akimwambia Mhazini baada ya kummwagia maji kusherehekea siku yake ya kuzaliwa ambayo ilichagizwa na ushindi wa timu ya SVSC

wachezaji wa SVSC na wa Wazee sports wakifurahia kwa pamoja baada ya michuano hii kufungwa na ikiwa imeendwa vizuri kabisa





Kabla ya mchezo kuanza kwa hisani ya Blogger..

Mhazini wa SVSC Dr Shukia pia  ilikuwa siku yake ya kuzaliwa. Hapo akimwagiwa maji  na wapenzi na wanachama wa SVSC kama ishara ya furaha ya kuzaliwa na kwa ushindi wa timu ya SVSC kwa kutwaa kombe mara tatu mfurulizo

Mchezaji mwenye misuri minene Salvatory Malongo ambaye alitoa pasi kwa Dr. Mwinyi ambaye alifunga goli la kuongoza katika ushindi wa magoli 2-0 ambapo SVSC walichukua ubingwa kwa miaka 3 mfurulizo

Arbert Sengo Mfungaji wa goli la pili ambalo lilipoteza kabisa matumaini ya Wazee Sports  kupata ushindi

Musa Siwiti akionesha ufundi katika kumiliki mpira kabla ya mchezo kuanza katika uwanja wa Taifa (shamba la bibi)

Mshambuliaji mwenye misuri Benson Hagai akichezewa mazambi na beki wa Wazee Sports na ilikuwa faulo ambayo haikuzaa matunda...

Beki hatari Joseph Mwasenga (Ayala) akimuacha mshambuliaji wa Wazee Sports na kuambaa na mpira katika uwanja wa Taifa (Shamba la bibi) ambapo SVSC walishinda 2-0 na kuchukua ubingwa...


MICHUANO YA PASAKA: MECHI YA UTANGULIZI WAZEE SPORTS WAWAFUNGA WAZEE WA SURVEY VETERAN 2-1

 
 Kabla ya mechi ya fainali kulikuwa na mechi ya utangulizi iliyopigwa kati ya Wachezaji wenye umri zaidi ya miaka 50 kwa kila timu ambapo wazee Sports walishinda kwa magoli 2-1

John MBitu (Benteke) katika maandalizi ya mchezo wa utangulizi








Kutoka kulia Dr. Rasul Ahmed, Pius na Bruce Herman wakipasha misuri moto kabla ya mchezo wa utangulizi ambazo SVSC ililala lwa mabao 2-1






MICHUANO YA PASAKA: WAZEE SPORTS CLUB YATOKA SARE NA TANZANIA STARS


Timu ya Wazee Sports Club wakiwa wamechanganyika na wenyeji wao Survey Veterans wametoka sare ya kufungana magoli 2-2 na Timu ya Tanzania Stars ambayo inaundwa na wachezaji wa zamani wa timu ya taifa na vilabu vikubwa nchini Tanzania. Mchezo uliochezwa katika uwanja wa nyumbani wa Survey Veterans (OT) uliopo chuo kikuu Ardhi.


Wachezaji wa Timu ya Tanzania Stars wakifanya mazoezi kabla ya mechi kuanza



John Mbitu akiwa na kaka yake kabla ya mchezo kuanza



Mchanganyiko wa Wazee Sports na SVSC wakifanya mazoezi kabla ya mchezo kuanza









Timu ya wazee na Survey Wakiwasalimia Tanzania Stars kabla ya mchezo kuanza

Mchezo ulikuwa mzuri na wakiistarabu kwa kuzingatia umri na aina ya wachezaji walioshiriki katika mchezo huu.