Friday, 3 April 2015

TIMU YA SURVEY VETERANS YALAZIMISHWA SARE NA TIMU YA KOMBAINI YA VETERANS YA ZANZIBAR





Ilikuwa penati iliyopigwa kwa ufundi mkubwa na Katibu mkuu wa SVSC Bw, Suleiman Mgaya iliipatia timu ya Survey  Veterans goli la kuongoza katika kipindi cha kwanza katika mechi iliyochezwa usiku katika uwanja wa Amani mjini Zanzibar baada ya Mshambuliaji mwenye misuri minene kuangushwa katika eneo la hatari na mwamuzi kuamua ipigwe penati

Kipindi cha pili kilianza kwa kila timu ikifanya mabadiliko mbalimbali ambapo Timu ya kombaini ilipata goli la kusawazisha, lakini timu ya SVSC inabidi ijilaumu yenyewe baada ya kukosa mabao matatu ya wazi baada ya straika wake hatari Richard Mbunga akiwa yeye na golikipa wa kombaini aligongesha mwamba wa juu na mpira kumkuta Edwin Mfanga ambaye naye aligongesha mwamba na mpira kutoka nje.

Katika harakati za kuokoa mpriga Beki hatari wa kutumainiwa wa SVSC , Ahmed Salumu aligongana na golikipa wake na mshambuliaji wa timu ya Kombaini na kumuumiza puani na kukimbizwa hospitali baada ya hali yake kuwa siyo nzuri. Hadi kipenga cha mwisho kinapulizwa na mwamuzi aliyeinyima penati ya wazi timu ya SVSC magoli yalikuwa sare ya goli 1-1

MATUKIO KATIKA PICHA , ZIARA YA TIMU YA SURVEY VETERANS- MJINI ZANZIBAR

"Safari ilianzia hapa"

Enock naye alikwepo!

"Beki hatari naye pia alikuwa mmojawapo

"Chapati kuku  tamu shehe!!" ndivyo inavyoelekea  Katibu mkuu Bw, Suleiman Mgaya akimwambia Mwl mkuu wa SVSC Bw, Ramadhan Bomba  wakiwa wanapata  Kifungua kinywa baada ya kuwasili Zanzibar

"Ndani ya "Chai Maharage kutoka Bandarini"


"Ndiyo mara yangu ya kwanza kufika Zanzibari"




"Kitu Ukwaju siyo mchezo"

"Kipapatio"

Hii chai mbona tamu sana ......cha tatu hiki !!!!"Sha-Makala"


Rais wa Wazee Veterans akitukaribisha Zanzibar

Wachezaji na wakimsikiliza Rais wa Wazee Veterans hayupo  kwenye picha baada ya kuwasili katika hoteli ambayo waliiandaa kwa ajili yetu

"Historia Imeandikwa"


Sha-Mande:"We umewahi kucheza uwanja huu?
Sha-Makala: Sijawahi na sijui kama ntacheza maana ni maji ya jioni haya sasa!!!
Sha-Mande: Leo Historia itaandikwa leo

Maandamano ya Michezo ya Pasaka

Juu na chini , ni wachezaji wa SVSC wakishiriki katika maandamani ya pasaka mjini Zanzibar










TIMU YA SURVEY VETERANS SPORTS CLUB ZIARANI ZANZIBAR KWA AJILI YA MICHEZO YA PASAKA



Timu ya SVSC imeondoka leo jijini Dar es salaam kwa boti ya Kilimanjaro kwenda Zanzibar kwa ajili ya michezo ya Pasaka. Timu imewasili salama visiwani humo na kupokelewa na wenyeji wao Wazee Veterans ya Visiwani humo.Timu imeondoka na wachezaji 23 na viongozi 4 ambao ni Bw. Suleiman Mgaya (Katibu Mkuu Mkuu wa msafara) Richard Shukia ( Mhazini mkuu), Ramadhani Bomba Mwalimu wa timu na Benson Mwemezi M/Mhazini.

Wachezaji walioongozana na timu ni pamoja na Golikipa hatari Kilibe Jumbe,Athuman Kione, Pius Joseph, Mohamed adam (M/kiti wa Mashindano, Josephat Edmund, Faraji Ghalib,Peter Ngasa (Captain), Steven Nyenge, Beki hatari Osca Mwambinga. Wengine ni Frank Gaspar, (mjumbe kamati ya nidhamu) Said Mahoka, Enock James, Ally Mgaya (mjumbe kamati ya ufundi), David Kiganga,Said Omary,Musa Siwiti (mjumbe kamati ya nidhamu (blogger), Ahmed Salum, Richard Mbunda na Macocha Tembele.
Timu ikiwa visiwani humo, itashiriki michezo ya Soka, kuvuta kamba pamoja na Pool table. Timu inatarajia kurejea jijini Daresalaam tarehe 3/4/2015 na ushindi wa michezo yote iliyotajwa hapo juu baada ya kufanya mazoezi ya kutosha.