Monday, 23 July 2018

TANZIA


Benjamin Magadula (katikati)
Mchezaji na mwanachama mwenzetu wa Survey Veterans Bw Benjamin Magadula amefiwa na mama yake mzazi aliyekuwa amelazwa katika hospital ya Bugando mwanza
.. Mungu ailaze roho ya marehemu mama yetu mahali pema poeponi Amina

Sunday, 22 July 2018

SURVEY VETERANS YAFUNGWA KWA TAAAAABU!! SANA NA NSSF


Picha: Kutoka Maktaba
SVSC Katika uchovu mkubwa ikitokea kuwafunga Stop Over veterans magoli 7-0 na pia kwa huzuni kubwa walionayo baada ya mchezaji mwenzao Benjami Magadula kufiwa na mama yake mzazi, ilifungwa kwa taaabu sana na timu ya NSSF kwa magoli 3-0. SVSC iliyocheza vizuri muda wote, bahati haikuwa yao baada ya kupata nafasi nyingi ila mashuti ya washambuliaji wake hayakulenga goli na mengine yaliokolewa na golikipa wa NSSF ambaye alifanya kazi kubwa sana kuiokoa timu yake.

Picha zote kutoka maktaba ya Timu ya SVSC
Kutoka kulia Shaban Seleman. Bilauli T na Edwin kabla ya mchezo kuanza

Kaptain wa Timu ya SVSC Mohamed Adam wapili kutoka kushoto akitoa maelekezo ya mwisho kuelekea mchezo


Jeff kulia na Edwin kushoto wakiwa katika chumba cha kubadilishia mavazi

Ekingo akitoka kwenye chumba cha kubadilishia mavazi tayari wa mchezo





STOPOVER VETERANS YAPIGWA KIPIGO CHA MBWA MWIZI NA SURVEY VETERANS


Kipigo kikali kutoka SVSC kiliwapelekea Timu ya Stop Over Veterans kumuomba mwamuzi waliekuja nae kumaliza mpira kabla muda wake baada ya kufungwa magoli 7-0. Magoli mawili yaliyofungwa na mshambuliaji hatari Musa siwiti, Magoli mawili yaliyofungwa na Peter Simon pamoja na magoli mengine matatu yaliofungwa na washambuliaji wengine, yalitosha kuwanyong'onyesha timu ya Mwanachama Mwenzetu bilauri T. na kuwafanya waondoke vichwa chini katika uwanja wa nyumbani wa SVSC,.



Kutoka kulia: David Kiganga, Benjamin Magadula na James Kabambo kushoto kabla ya mchezo kuanza

Maandalizi kabla ya mchezo