Wednesday, 22 August 2018

TIMU YA BREAK POINT YAKIONA CHA MOTO KWA SURVEY VETERANS


Bw. John Mbitu "Benteke au Morata" wa pili kutoka kushoto waliosimama na Timu yake ya Friends of Break Point kabla ya mchezo ambapo walichapwa magoli 3-0 na timu ya Survey Veterans
Timu marafiki ya Mwanachama wa SVSC  mwenzetu Bw. John Mbitu "Benteke" ilijikuta katika wakati mgumu sana baada ya kupapaswa magoli 3-0 na timu ya SVSC .




Morata kama anavyojulikana kwnye timu ya Friends of Breakpoint akipasha mwili moto kabla ya mchezo kuanza.

FRIENDS OF BREAKPOINT YAPAPASWA NA SURVEY VETERANS


Paschal Fumbuka wa mbele kulia, Mfungaji wa magoli ya SVSC na wachezaji wenzake wakimsikiliza mwalimu hayuko pichani kabla ya mchezo kuanza
Ilikuwa zamu ya Timuya Friends of Breakpoint Kupapaswa na Timu ngumu , timu hatari , timu yenye wachezaji wengi na timu pekee katika jiji la DSM inayocheza dakika 120 katika kila mechi Timu ya Survey Veterans. Magoli ya Michael Fumbuka  yalitosha kabisa kupeleka kilio katika timu ya mwanachama mwenzetu John Mbitu (Mfadhili wa timu ya Breakpoint) anayejulikana kwa jina la kimichezo "Benteke" kwa upande wa SVSC na " Morata" kwa upande wa Breakpoint. Pamoja na kuingiza marafiki zake vijana lakini ilikuwa ngumu sana kwa wazee wazoefu wa SVSC. 



Mwalimu Bomba mwenye jezi ya Yanga akitoa maelekezo ya mwisho kabla ya mchezo kuanza.

Hassan Mussa kulia, Dkt Mbunda na husein wakimsikiliza mwalimu wakati wa mapumziko. (Dr Mbunda akitoa matope kwenye kiatu chake tayari kwa kipindi cha pili)

Wakati wa Mapumziko timu ikimsikiliza mwalimu.

Mjumbe kamati ya Ufundi Ally Mgaya akitoa tasmini ya mchezo kipindi cha mapumziko kushoto kwake Kasimu Ramia  akimsikiliza kwa makini.