Tuesday, 22 December 2015

GASABILE VETERANS YAKIONA CHA MOTO KWA SURVEY VETERANS


Timu ya SVSC ilitoa kipigo kikali mbele ya Gasabile Veterans katika uwanja wao kwa kuibugiza magoli 4-1. SVSC ikicheza katika ubora wake, iliwachukua dakika 15 kupata goli la kuongoza kupitia beki wake hatari mwenye misuri minene na mashuti makali Ahmed Salumu baada ya kuwapita mabeki wa Gasabile na kuachia shuti kali la guu la Dhahabu na kuipatia SVSC goli la kuongoza. baadae Gasabile walisawazisha na hadi timu zinaenda mapumziko mabao yalikuwa 1-1.

Kipindi cha pili kilianza kwa kila timu kufanya mabadiliko na baadae kidogo timu ya SVSC ilipata magoli mawili ya haraka haraka kupitia fowadi wao hatari Dulla. Goli la nne liliwekwa kimiani kiufundi na winga hatari ambaye alikuwa katika kiwango bora katika mechi hiyo Musa Siwiti baada ya kuunganisha krosi safi iliyopigwa na beki mahili Ahmad Shaweji. Hadi mwisho wa mchezo SVSC walishinda kwa goli 4-1


Sunday, 13 December 2015

TIMU YA VIJANA YA UKAGUZI YAIFUNGA SURVEY VETERANS GOLI 5-1


Timu ya vijana ya Ukaguzi imeifunga Survey Veterans goli 5-1 katika uwanja wake wa nyumbani katika mchezo uliochezwa jumapili tarehe 12/12/2015. Timu ya Vijana ya Ukaguzi ikichezesha Vijana wengi tofauti na Survey Veterans, iliwachukua dk 20 kupata magoli ma nne.Hii inatokana na uwezo wao kama vijana ukilinganisha na wazee wa Survey Veterans.Hadi timu zinaenda mapumziko, Timu ya vijana ya Ukaguzi ilikuwa inaongoza kwa goli 4-0.

Kipindi cha pili kilianza kwa kila timu kufanya mabadiliko na kila timu kupata goli moja moja. Hadi mwisho wa mchezo Timu ya Ukaguzi ilishinda goli 5-1.

MATUKIO YA PICHA KATIKA MCHEZO HUO

Winga hatari Musa Siwiti muda mfupi kabla ya mchezo kuanza

Kutoka kulia Dulla mshambuliaji hatari, T.Bilauli, Kiganga D., Beki hatari Dkt Kibasa D, Capt Ngassa, Beki hatari Ahmed Salum, Beki ya kati James Kabambo na Winga hatari Musa Siwiti wakimsikiliza mwalimu hayupo pichani kabla ya mchezo kuanza

Beki hatari ikipasha misuri moto kabla ya mchezo kuanza


Beki visiki Ahmed na Dkt Kibasa wakipasha misuri moto kabla ya mecho kuanza

Kutoka kulia James Kabambo, Bilauli na Kiganga kabla ya mchezo

Captain Ngassa akipasha misuri moto kabla ya mchezo kuanza

Winga ya kuingia nazo" Mbunda akipasha misuri moto kabla ya kchezo kuanza....


John Mbitu "Benteke" akipasha msuri moto kabla ya game kuanza.....


Kwenye maandalizi ya mwisho.

TIMU YA LUGALO VETERAN YALAZIMISHA SARE YA 3-3 KWA SURVEY VETERAN


Ilikuwa mchezo mkali katika uwanja wa Lugalo Veteran  zilipokutana timu ambazo zinaelekea kuwa ni wapinzani wa muda mrefu. Mara ya mwisho zilipokutana katika uwanja wa Nyumban wa Survey Veteran, timu ya Lugalo ilishinda wa goli 3-2 na mara hii ilijaribu kutaka kuendeleza uteja lkn mchezo ulikuwa mgumu kwao baada ya kujikuta wakilazimisha sare.

Ilikuwa ni timu ya Lugalo iliyoanza kupata goli kipindi cha kwanza lakini iliwachukua dakika 15 tu Survey Veteran kusawazisha kupitia adhabu ndogo iliyopigwa na Beki hatari Ahmed Shaweji baada ya winga wao hatari Musa Siwiti kufanyiwa madhambi mita 20 toka langoni mwa Lugalo veterans.

Timu zilienda mapumziko zikiwa sare ya goli moja kwa moja. Lugalo walipata goli la pili na Survey kusawazisha baadae kupitia kona mujarabu ilipigwa na winga hatari Musa Siwiti na kumkuta Ahmad Shaweji alioukwamisha mpira wavuni.
Baadae timu zote zilifanya mabadiliko na kufanikiwa kupata magoli. Hadi mwisho wa mchezo SVSC 3 na Lugalo Veteran 3.

Tuesday, 29 September 2015

MATUKIO YA PICHA KATIKA MECHI YA MAGOGONI VETERANS NA SURVEY VETERANS

kutoka kushoto Banyikwa, Bluce, Mohamed Adam na James Kabambo

Musa Siwiti na Bluce kabla ya mechi kuanza

Mwl Bomba mwenye suruali  akitoa maelekezo ya mwisho kabla ya mchezo






Magogoni veterans wakifanya maandalizi ya mwisho kabla ya mchezo kuanza




Monday, 28 September 2015

UJIO WA BRUCE HELMAN WANOGESHA USHINDI WA SVSC

Ujiowa beki mbili wa timu ya Survey Veterans kutoka Marekani ulinogesha ushindi wa goli 4 kwa bila dhini ya Magogoni Veterans.Kma kawaida ikicheza katika uwanja wake wa nyumbani iliwachukua dk 15 kupata goli lake la kwanza.


Bruce Helman wa kwanza  kutoka kulia waliochuchumaa (white Man) aliisaidia timu yake kupata ushindi wa magoli 4-0 dhidi ya Magogoni Veterans 

Friday, 18 September 2015

MASALIA YA BOMBA DAY

 Baada ya sherehe ya kumpongeza Mwl Bomba masalia ya pesa yalisalia na Mwenyekiti kumkabidhi Mwl kama matukio ya picha yanavyoonesha
.... Dah Asante sana Mwenyekiti..... Ndiyo inaonekana Mwalimu Bomba alikuwa akisema....M/kiti wa SVSC Bw. Peter Mweta akimkabidhi masalia ya siku ya Bomba day Mwl Ramadhan Bomba kiasi cha pesa Tsh 60,000/= pesa ambazo zilibaki katika matumizi ya siku ya sherehe huku katibu wa SVSC Bw. Suleiman Mgaya akiangalia kwa karibu.

MATUKIO KABLA YA MCHEZO

D. Kiganga kushoto na Carlos Kulia wakipasha misuri moto kabla ya game

James Kabambo kushoto B. Magadula katikati na D Kiganga Kabla ya Mechi

Sbaban K, na 32 B. Magadula a 8 na wachezaji wengine kabla ya mechi



Kabla ya Mechi

Hamis Gaga kulia, Carlos ,D Kiganga na Moses Kabla ya Mechi

Golikipa hatari  Yona mwenye jezi nyekundu, Jumanne katikati na Dulla kabla ya mechi

Naseeb kulia, Magadula katikati na Gaga wakipasha misuri kabla ya mechi

Captain Mohamed Adam, kulia Said sise katika na Mussa Hassan wakipasha misuri moto kujiandaa na mchezo


John Mbitu kushoto, Peter Mweta (Mwenyekiti wa SVSC na Sbhaban K wakipasha misuri kabla ya mechi



NSSF VETERANS YALAZIMISHA SARE KWA SVSC


Timu ya kuungaunga ya NSSF ikiwa na mamluki kutokea timu pinzani iliweza kulazimisha sare ya goli 1-1 kutoka kwa timu ya Survey Veterans .
Ilikuwa ni NSSF iliyoanza kufunga goli kipindi cha pili. Mshambuliaji hatari wa SVSC Innocent Lyimo (Mangi) akiingia kipindi cha pili aliweza kuisawazishia timu ya SVSC  Veterans. NSSF pamoja na kufanya mabadiliko machache, waliweza kuimarisha basi lao na kuhakikisha washambuliaji wa SVSC hawapenyi ngome iliyokuwa ikiongozwa na beki Mamluki Ally Mgaya. Hadi mwisho wa mchezo SVSC 1 na NSSF 1.
MATUKIO YA PICHA KABLA NA BAADA YA MCHEZO

Sunday, 30 August 2015

ZAWADI YA TIMU KWA RAMADHANI BOMBA


Timu ya SVSC katika kufahamu umuhimu wa Mwl, kwa kushirikiana na Mwl Bomba walikubaliana tumnunulie king'amuzi cha Azam kama zawadi ya timu kwake,
Matukio ya picha hapo chini yanaonesha mahabidhiano hayo.
M/M/kiti Dkt. Rasul akikabidhi king'amuzi kwa Mwl Bomba kama zawadi ya timu katika siku Bomba Day huku Capt Mohamed Adam akishuhudia kwa karibu.


Bw, Ramadhani Bomba akiangalia kwa furaha zawadi yake 







SHEREHE YA KUADHIMISHA BOMBA DAY ETINA BAR & RESTAURANT

Baada ya mchezo wa kuadhimisha siku hii muhimu, kulikuwa na sherehe iliyoandaliwa na wanachama kwa ajili ya kumpongeza mwalimu kwa kazi kubwa anayoendelea kuifanya katika timu. MATUKIO YA PICHA ANAONESHA,
Katibu Mkuu Suleiman Mgaya , Kaimu Katibu Shabani K. aliyeshika simu na Kaimu Mwenyekiti Dkt, Rasul wakiwakaribisha wapenzi na wanachama katika sherehe ya kuadhimisha siku ya Bomba day Etina Bar &Restaurant.

David Kiganga akifungua champagn kuashiria kuanza kwa sherehe hiyo.

Peter Ngassa (Capt) kushoto,John MBitu  katikati na Misheki  kulia wakifuatilia kwa makini malezo ya Katibu.

....Kaimu Mhazini Benson Mwemezi kulia na Capt Adam Zengwe wakisikiliza hotuba ya Katibu ....

Ramadhani Bomba kushoto akitoa neno la shukrani kwa wapenzi na wanachama wa SVSC hawapo pichani katika siku ya kuadhimisha siku ya Bomba Day huku  M/M/kiti Dkt Rasul akifuatilia kwa makini.

Ikafika muda wa msosi kama ambayo katibu Suleiman Mgaya , Joseph Mwasenga wanagonga Menu.


John Mbitu, Hgai, Misheki na wengine wakiwa wanapata Menu

Ramadhan Bomba ambaye ilikuwa siku yake muhimu akipata msosi

Dkt Rasul akipata msosi siku ya Bomba Day


.....KIMEISHA......

Blogger  Musa Siwiti alikuwa Kazini kuhakikisha Mambo yote yanarekodiwa kwa usahihi na kuingizwa katika blog ya Timu...



Blogger wa Timu Musa Siwiti kushoto, Ahmad Shaweji katikati na Mahoka wakiwa wanapata Msosi katika siku ya Bomba day