Wednesday, 28 December 2016

SURVEY VETERANS YANG'ARA MKOANI TANGA




Mpira kazi!!

Beki timu ya Upinzani akimsukuma Iddy Ngaoneka huku Beki hatari Shukia akiwa tayari kuondoa mpira katika eneo la hatari
Baadhi ya wachezaji waliosafiri na timu mkoani Tanga; kutoka kushotowaliokaa Franka Gaspa, Said Seif. Waliosimama kutoka kushoto; Ahmad Shaweji, Peter Ngassa,Richard Shukia,Iddy Ngaoneka,Mohamed Adam,Steven Nyenge,Emmanuel Ekingo na Ally Mgaya.


SURVEY VETERANS YAFANYA VIZURI MICHEZO YA BONANZA TANGA

Steven Nyenge (stevovo) akiuweka mpira kwenye imaya yake huku Arbart Sengo akimsogelea kwa msaada huku Ekingo na Mohamed Zengwe wakiwa wanawalinda wachezaji wa upinzani wasilete madhara. SVSC walishinda 2-0
Dah.... Game tight... Ally Mgaya kushoto anaonesha anamwambia Kept Peter Ngasa kulia


.....Unaweza ukafa......Mohamed Adam akiwa amechoka baada ya mchezo kumalizika na SVSC kushinda 2-0


 Ally Mgaya kushoto na Richard Shukia akifatilia mchezo baada ya kupumzishwa,....
Muuaji wa magoli ya SVSC Arbart Sengo akiwaeleza wachezaji wenzake hawapo pichani jinsi ya kuwatoka mabeki wa timu Pinzani

Kepteni wa mchezo huo Ahmad Shaweji akiwa anafuatilia mchezo baada ya kupumzika

Golikipa Shah Pele aliyevua shati, Godwin Ekingo aliyekaa kwenye kiti, Mnyama Iddy Ngaoneka kulia na Mohamed Zengwe wakijadili jambo baada ya mchezo



Frank Gaspar Baada a kupumzishwa akitoa maelezo kwa wachezaji wengine ..

Mtaalamu wa pass uwanjni Stevovo Nyenge bada ya mchezo kumalizika

Arbart Sengo akijiandaa kumtoka beki wa timu pinzani huku Iddy Ngaoneka akiwa karibu kwa msaada

Golikia wa Mashindano Shah Pelle akiokoa mchomo kutoka kwa mshambuliaji wa timu ya upinzani...

Monday, 19 December 2016

KAWE VTERANS YALAZIMISHA SARE KWA SURVEY VETERANS


Timu ya kawe Veterans ilijitahidi kulazimisha sare ya bao 3-3 baada ya mechi kali ya kirafiki iliyopigwa uwanja wa Survey.



























Saturday, 13 August 2016

NSSF VETERANS YAPIGWA GOLI 2-1 NA SURVEY VETERANS KATIKA UWANJA WA JK PARK

Timu ngumu mkoa wa  Dar es salaam Survey veterans  jana ilipeleka kilio tena kwa wenzao wa NSSF Veterans walipojaribu kujiuliza tena baada ya mechi ya awali kutoka sare na SVSC kwa kuwafunga bao 2-1. Pasi nzuri kutoka kwa foward hatari Benson Mwemezi ilimfikia Winga hatari Musa Siwiti na kuukwamisha mpira wavuni na kuandika bao la kuongoza katika dakika 15 ya kipindi cha kwanza.
Pia winga hatari Musa Siwiti nusura aipatie SVSC bao la pili pale shuti lake kali lilipogonga mwamba na kutoka nje baada ya kona nzuri iliyochongwa na James Kabambo. Hadi timu zinaenda mapumziko SVSC ilikuwa inaongoza kwa goli 1-0.
Kipindi cha pili kilianza baada ya kila timu kufanya mabadiliko na SVSC walifanikiwa kupata goli la pili lililofungwa na Humprey Machota baada ya kuwashinda nguvu walinzi wa NSSF Veterans na kuukwamisha mpira wavuni. Dakika 10 kabla ya mpira kumalizika NSSF walipata bao la kufutia machozi kupitia winga wao hatari baada ya kumalizia mpira uliotemwa na golikipa wa SVSC. Mpira ulianza saa mbili usiku na kumalizika saa tatu na nusu usiku.

Na Blogger wako.....  Sha_makala

Uwanja wa JK Park unavyoonekana wakati wa usiku ambapo timu ya NSSF ilipomenyana na tina ngumu mkoa wa Dar esa salaam Survey Veterans na kukubali kibano cha bao 2-1

Mchezaji Mwenyeji Dominic Mbwete mwenye jezi ya njano, akiteta jambo na washabiki wa Survey Veterans kabla ya mchezo kuanza ambapo Timu yake ililala kwa bao 2-1



TIMU YA SURVEY VETERANS YASHINDA GOLI 2-1 MICHUANO YA 88 MKOANI MOROGORO

Mchanganyiko wa Timu ya SVSC na Reli Veterans kabla ya mchezo kuanza

Timu ya Survey Veterans ilifanya ziara ya kimichezo mkoani Morogoro na kucheza mechi ya kirafiki na Timu ya Reli Veterans ya Morogoro na kuifunga goli 2.-1. Hadi timu zinaenda mapumziko Timu ya Reli Veterans ilikuwa inaongoza kwa goli 1-0. Goli la kusawazisha lilifungwa na Godwin ekingo na goli la pili na la ushindi lilifungwa na Captain Peter Ngassa baada ya kuiadaa ngome ya wapinzani na kufunga goli la kusawazisha.
LISTI YA WACHEZAJI WALIOILETEA USHINDI TIMU YA SURVEY VETERANS

  1. Shah (Golikipa)
  2. Innocent Lyimo
  3. Salum Mvule/Mbwete Dominic HT
  4. Charles Antipas
  5. Hamad Shaweji
  6. Mweta Peter/Dulaa (Dk 32 maumivu ya paja)
  7. Frank/Kiganga Dk 56
  8. Ngassa Peter (Capt)
  9. Ekingo
  10. Suleiman Mgaya
  11. Japhet/Momo Cisse
SUB ZINGINE
Suleima Mgaya /Koba
Mwl Ramadhan Bomba akitoa maelekezo ya mwisho kabla ya mchezo, Kutoka kulia Dominic Mbwete,Godwin Ekingo, Suleiman Mgaya (katibu),Charles Antpas, Capt Peter Ngasa,Innocent Lyimo, Sisse Momo, David Kiganga Dulla na Peter Ngasa
Timu zote mbili zikisalimiana kabla ya mchezo kuanza



"Wanaongoza, Siyo mbaya ndiyo mchezo, ila bado nafasi tunayo tukitulia...." Maneno ya mwalimu Ramadhani Bomba baada ya kipindi cha kwanza kumalizika na Reli Veterans walikuwa wanaongoza kwa goli 1-0

Dah... Game "tight" ndiyo inanyooneka wachezaji wakijadili Frank Gasper mwenye raba, Charles aliyevua jezi, Ekingo anayevaa kiatu waliosimama Peter Ngassa ,David Kiganga na Suleimani Mgaya na wengine katika kipindi cha mapumziko

Sunday, 29 May 2016

SURVEY VETERANS SPORTS CLUB YAFANYA ZIARA YA KIMICHEZO JIJINI MBEYA

SURVEY VETERANS SPORTS CLUB YAFANYA ZIARA YA KIMICHEZO JIJINI MBEYA
Kikosi kamili kilichowakilisha Mbeya kutoka kulia walioinama, Osca Mwambungu,Mohamed Adam (Captain) Ahmed Shaweji,Suleiman Mgaya,Innocent Lyimo na Benson Hagai. kutoka kushoto waliosimama, Dkt Rasul Ahmed,Arbet Sengo,Steven Nyenge,Peter Mweta na Ramadhan Bomba (Mwalimu wa Timu)
Timu ya mpira wa miguu ya Survey Veterans Sports Club imefanya ziara ya michezo ya kirafiki jijini Mbeya baada ya kupokea mwaliko kutoka timu Mwenyeji ya Mbeya Veterans. Timu iliondoka jijini Dar esa laam kwa Ndege ya Fastjet  siku ya ijumaa ikiongozwa na Mwenyekiti Peter Mweta, M/M/kiti Dkt Rasul Ahmed, Katibu Mkuu Suleimani Mgaya, K/Katibu Shabani Seleman, Mwalimu wa Timu Ramadhani Bomba Capt Mohamed Zengwe na wengine. Timu ilifika salama jijini Mbeya na kupokelewa na wenyeji na kupelekwa hotelini.Timu ilicheza  michezo miwili ya kirafiki na  timu B ya Mbeya City na kufungwa magoli 2-1. na Mchezo wa pili ilicheza na wenyeji wao Mbeya Veterans na kutoka sare ya goli moja kwa moja   Timu ilikaa jijini mbeya kwa siku mbili na kurejea Dar es salaam siku ya jumapili tarehe 29/05/2016

MATUKIO YA PICHA KATIKA ZIARA HIYO


Arbart Sengo kutoka kushoto, Innocent Lyimo na Benson Hagai golikipa katika maandalizi ya mwisho kabla ya mchezo

Katibu Suleiman Mgaya kushoto na Innocent lyimo kulia  kabla ya mchezo

Dkt Rasul Mwalimu wa timu na Golikipa hatari katika maandalizi ya mwisho kabla ya mchezo
Mbwiga wa Mbwiguke alikuwa mchezaji mwalikwa katika timu ya SVSC katika mchezo wa kwanza