Friday, 29 December 2017

MWALIMU BOMBA KATIKA KAZI YAKE YA KILA SIKU


Mwalimu Ramadhani Bomba amekuwa ni mtu wa pekee katika timu ya SVSC. Ni mwalimu wa nidhamu, mwalimu wa mpira na mambo mengine yanayohusu maisha binafsi. Hii ni pale ambapo mchezaji anapoenda kinyume anamrekebisha kwa kumuonya na kumfanya awe mchezaji mzuri. Baada ya Peter Simon kukengeuka Mwalimu pamoja na wanamichezo wengine walimtaka kujirekebisha na kwenda sawa na falsafa ya Survey Veterans ya Upendo, uvumilivu, kuheshimiana kati ya mtu na mtu uwanjani na nje ya uwanja. Tunampongeza sana Mwalimu Bomba

SURVEY VETERANS GET TOGETHER PARTY YAFANA


Ilikuwa siku muhimu sana kwa wana Survey wote, Wapenzi, wanamichezo na wanachama kwa ujumla pale ambapo walikusanyika kwa pamoja kwa ajili ya kusherehekea siku kuu ya krismas. Ni utaratibu ambao wamejiwekea kila panapokuwa na sikukuu kubwa kama Pasaka, krimas na Idd.

Tuesday, 26 December 2017

NSSF YALAZIMISHA SARE NA SURVEY VETERANS


Timu ya NSSF ililazimisha sare ya magoli 2-2 na timu ngumu ya SVSC. Timu hii ya NSSF imekuwa mpinzani mkubwa sana kwa SVSC kwa mwaka huu maana tumekutana mara tatu na mara zote tumetoka sare.




Captain Peter Ngasa Mwenye notebook mkononi akitoa maelekezo kwa wachezaji kabla ya mchezo kuanza. aliyekaa chini ni Chacha kibago

Sunday, 17 December 2017

INNOCENT LYIMO: BINGWA WA MBIO ZA MITA 100 BONANZA LA NEIGHBOURS

Innocent Lyimo akipokea zawadi yake ya ushindi wa mbio za mita 100 kutoka kwa mchezaji mwenzake John mbitu katika bonanza la ujirani mwema

ALBERT KAJALA SENGO MFUNGAJI BORA WA MASHINDANO YA BONANZA

Albert Sengo mfungaji bora wa bonanza akiwa na watoto waliokuja kushangilia na kufuatilia michezo hiyo

MATUKIO YA PICHA KATIKA BONANZA HILO

Hamis Gaga (Gagarino) akipokea zawadi yake ya uchezaji bora wa mechi ya kwanza





















SURVEY VETERANS MABINGWA BONANZA LA NEIGHBOURS


Timu  hatari ya SVSC iliweza kutwaa ubingwa wa Bonanza siku ya jumamosi katika uwanja wa Neighbour's Madale Mivumoni kwa kuzifunga timu zote zilizoshiriki bonanza hilo. Mechi ya kwanza SVSC ilicheza na Madale Veterans na kuwafunga magoli 4-2,huku magoli mawili yakifungwa na Albert Sengo, Hamis Gaga (gagarino) akifunga goli moja na goli la nne likifungwa na Benjamin Magadula.

Mechi ya pili tulicheza na Wenyeji Neighbours Veterans na kuwafunga goli moja liliwekwa kimiani na Chacha Kibago. Mechi ya tatu SVSC ilishinda kwa magoli mawili magoli yote yakifungwa na  Albert Sengo kwa kumalizia shuti kali la Musa Siwiti ambalo golikipa alilitema.

Mchezo kwa ujumla ulikuwa mzuri na timu ilicheza kwa uwelewano mkubwa sana. Pia timu ya SVSC ilitoa washindi wawili kwenye mbio za mita 100. Innocent Lyimo akichukua zawadi ya Ushindi wa kwanza na Joseph Mwasenga akichukua ushindi wa tatu.
Innocent Lyimo aliyevua shati akipokea zawadi yake ya mshindi wa kwanza wa mbio za mita 100 baada ya kuibuka mshindi kati ya washiriki 8 walioshiriki mbio hizo

Pia Golikipa namba moja Sha_Pelle alichukua golikipa bora wa mechi ya kwanza na Hamisi Gaga alichukua uchezaji bora mechi ya kwanza
Golikipa bora wa bonanza  Sha_pelle akiwa hoi bada ya kumaliza mchezo wa kwanza na kuchaguliwa kuwa golikipa bora wa mashindano. Pia ni golikipa aliyefungwa goli moja tu katika michezo yote mitatu aliyocheza.

Monday, 11 December 2017

MATUKIO YA PICHA KATIKA KUSHEREKEA SIKU YA NDOA YA Bw. ALLY MGAYA

Bwana Harusi Ally Mgaya akiwana na Bw Frank Gasper wakiwa na nyuso za furaha baada ya kukamilisha kisomo ambapo SVSC ilikaribishwa kwa ajili ya chakula cha mchana.


Bwana harusi Ally mgaya akiwa amepozi baada ya kumaliza kisomo na ni Muda sasa wadau na majirani kupata chakula


Wadau wakijumuika pamoja kwa ajili ya chakula cha mchana







MJUMBE KAMATI YA UFUNDI WA SURVEY VETERANS AAGANA NA UKAPERA.


Mjumbe kamati ya ufundi wa SVSC, Bw. Ally Mgaya ameagana na ukapera baada ya kufunga ndoa na mchumba ake. ilikuwa siku kubwa na muhimu sana kwa Bw, Ally na familia nzima ya wana SVSC ambapo walijumika pamoja katika kumpongeza na kumtakia maisha marefu yenye furaha na amani.

MKISI FC YAPIGWA GOLI 7 NA SURVEY VETERANS


Timu ya Mkisi FC ilikiona cha moto pale ilipokubali kichapo cha goli saba bila kutoka tomu ya SVSC. Goli la kwanza la SVSc liliwekwa kimiani na beki hatari Dr Deusdedit Kibasa baada ya kupata pasi kutoka wa mshambuliaji hatari Musa siwiti. Magoli mengine yalifungwa na Silvatory Malongo ambaye alifunga kwa kupiga kichwa hatari kilichomshinda kipa na kutinga wavuni.. Pia Iddy Kaoneka ( Mnyama) alifunga magoli matatu na kunogesha ushindi wa timu ya SVSC.





Tuesday, 26 September 2017

WAHENGA SPORTS CLUB YAKIONA CHA MOTO KWA SURVEY SPORTS CLUB

 Timu ya wahenga Sports Club inayoundwa na waandishi wa habari za michezo toka vyombo mbalimbali vya habari zikiwemo Tv Magazeti na Radio, walikutana na dhahama pale walipobugizwa magoli 5-0 na Svsc. Alikuwa ni Dr. Mwinyi ambaye alifungua ukurasa wa magoli yakifuatiwa na magoli yaliyofungwa na Mh Ridhiwani kikwete, Hassan Musa na Moses. hadi mpira unaisha SVSC 5 na Wahenga hawakupata kitu.
Kiungo shabani Kambabhe na Frank Maria wakinyoosha viungo kabla ya mchezo kuanza

Captain Peter Ngasa kulia na Moses kushoto kabla ya mchezo kuanza

Wahenga Sports kabya ya mchezo kuanza