Monday, 19 October 2020

TFL BONANZA TCC CHANG'OMBE: SURVEY VETERANS YAINGIA FAINALI.

 

Mwenyekiti Survey Veterans  Bw. John Mbitu kushoto waliokaa wakifuatilia mchezo huku wachezaji wengine wa SVSC wakifuatilia kwa karibu

Timu ya Survey Veterans imeingia fainali ya Michuano ya Bonanza lililoandaliwa na TFL katika kuazimisha siku ya Kumbukumbu ya kifo cha Mwl Nyerere baada ya uitoa Timu ngumu ya Azam Veterans. Penati mbili zilizopanguliwa na golikipa hatari Kiribe Soso" zilitosha kuwaondosha Azam kwenye Michuano hiyo.

Golikipa Kilibe akidaka mpira uliopigwa na Winga hatari wa Azam Veterns.


Monday, 24 August 2020

MATUKIO KATIKA MCHEZO

From other Country... Jeff Jeff...


FLORIDA VETERANS YAILAZA SURVEY VETERANS

Kiungo mchezesha timu Shabani Kambabhe akitoa pasi kwa mwenzake hayupo pichani. SVSC ilifungwa magoli 6-5

Ikiwa imesheheni vijana wenye uwezo mkubwa, Timu ya Floria iliwafunga wazee wa Survey Veterans kwa magoli 6-5
Timu ya Survey Veterans waliosimama mstari wa mbele kutoka kulia ni Siasa ( Siabonga), Agogo, Mwemezi, Innocent Lyimo, Shabani Kambabhe, Richard Mbunda, Hamad Shaweji, Mkapa, Elly na Mwalimu Bomba. walioinama mstari wa kati ni golikipa Mbaga, Peter Simon, Gagarino, Batto, Michael Simbaulanga, Captain Peter Ngassa. Na waliokaa chini mstari wa mbele kutoka kushoto ni Magoti, Tresor, Nelson, Kilibe, Peter ndosa na Beki hatari.

Ticktack ...Peter Ndosa SVSC


….Gooo gogogoooooooo…… Macelo


Timu ya Florida Veterans

Wednesday, 22 July 2020

KIMARA VETERANS KIBONDE MBELE YA SURVEY VETERANS

Timu ya SVSC waliosimama kutoka kulia ni Trezoo, Baton, Simango, Elly, Siasa, Hamisi Shomari (gagarino), Innocent Kuzengwa, Nelly, Mkapa, Peter Ndossa na Mwl Bomba. Waliochuchumaa kutoka kushoto ni Golikipa William, Shevichenko, Peter Ngassa, Emmanyel mwandumbya, Kilibe Soso, Magoti, Michael Mvanga na Mussa Siwiti.

Timu ya Kimara Veterans ilijikuta katika wawakati mgumu baada ya kukubali kichapo cha magoli 4-3 mbele ya Timu Hatari SVSC.Magoli mawili ya Trezoo na Gagarino yalitosha kuwaangamiza timu pinzani ya Kimara Veterans.
Dr Magoti akipiga shuti kali lkn halikulenga goli huku Trezoo akimfuatilia kwa aribu...


Siabonga Siasa akimiliki mpira kwa kiwango cha juu sanaaa 

Gagarino akifunga goli la nne kukamilisha ushindi wa 4-3 huku mabeki wa upinzani wakiwa hawana la kufanya

Winga hatari Mussa Siwiti akielekea goli la hadui huku wenzake wawili wakiwa karibu kumsaidia 

Sunday, 12 July 2020

MIPANGO VETERANS YAILAZA SURVEY VETERANS

Timu ya Survey Veterans waliosimama mstari wa nyuma kutoka kushoto ni John Mbitu (Benteke), Bilaul, MOhamed Zengwe, Magoti, Iddi Ngaioneka ,Elly, S. Malongo, Faraji, na Peter Ndossa. Waliochuchuma kutoka kulia ni Rasul Ahmed, Emmanuel Mwandumbya, Joseph Mwasenga na Mussa Siwiti

Timu ya Mipango Veterans imeifunga timu ya SVSC magoli 4-3 katika uwanja wa Taifa.. Ikitangulia kwa magoli 3-0 hadi kipindi cha kwanza kumalizika, Survey Veterans ilikuja juu na kufunga magoli matatu kabla ya mpira kumalizika. Goli la kwanza la SVSC lilifungwa na Salvatory Malongo na mengine yalifyngwa na Butto na





Sunday, 8 March 2020

MATUKIO YA PICHA KWENYE MCHEZO HUU


Muuaji wa magoli mawili ya SVSC Benson Hagai akitambuka galuga la Beki wa Temboni Veterans na kuipatia timu yake goli la pili.


Mshambuliaji hatari Malongo katika harakati za kumpiga chenga beki......

ILIKUWA ZAMU YA TEMBONI VETERANS KUPATA KIPIGO CHA 4-2

Kikosi cha SVSC kutoka kushoto mstari wa mbele Malongo S, Simbaulanga S., Mbitu J, Shomari H, Kilibe S, Captain Ngassa na Omary M. Waliosimama  kutoa kulia ni Adam Zengwe,Innocent Lyimo,elvin Haule,Bilauri T, Hagai B na Shaban Kambabhe.

Benson Hagai, magoli mawili, Kelvin Goli moja na Button goli moja yalitosha kabisa kuwafundisha mpira timu ya Temboni Veterans. Ikicheza katika uwanja wake wa nyumbani SVSC ilikuwa katika ubora wake iiwa katika maandalizi ya Michuano ya Pasaka na Wazee Sports kutoka Zanzibar na maandalizi ya kuadhimisha miaka 20 toka kuanzishwa kwake.

Wednesday, 1 January 2020

SHEREHE YA KUUKARIBISHA MWAKA MPYA 2020


 Baada ya mechi ya kirafiki Timu ilikusanyika katika Bar ya Migombani kwa ajili ya kuapata supu ya pamoja.







TIMU MAGIGE YALALA MBELE YA TEAM DETAH

Timu Manager Madam Detah akiwa na Captain wake Mohamed Zengwe kabla ya mchezo kuanza.

Kama ilivyo kawaida kwa Timu ya Survey Veterans kusherehekea Siku kuu ya mwaka mpya kwa kucheza mechi za Wenyewe kwa wenyewe.  Timu Ziliundwa kwa kusaidia na Manahodha wa pande zote mbili Timu zilipewa majina ya wanachama Wenzetu ambao ni wanawake Dada Datah na Mama ambaye hutuhudumia juice wakati wa Mazoezi. Baada ya mpambano mkali timu ya Detah ilishinda goli 1-0 lililofungwa na Iddi Kaoneka (Mnyama ) kwa kwa njia ya penati baada ya Sise kufanyiwa madhambi kwenye eneo la hatari.
Kikosi Ushindi: kutoka kulia waliosimama Sahid Mahoka, Ahmad Shaweji, Momo, Shabani Kambabhe, Peter Mweta, Team Manager Madam Detah. Walioinama kutoka kulia ni Kelvin,Michael ,Makoye, Musa siwiti,Shevy,n Golikip Mwandumbya. Waliokaa chini ni Peter Ndosa na Mohamed Adam.

Timu Magigi waliosimama kutoka kushoto ni Team Manager Madam Magigi, Bilauri, Osca Kobby, Mwenyekiti John Mbitu, Peter Simon, Nyigu, Wiliam Golikipa, na waliochuchumaa ni Mzee ndugulu kushoto, Batton, Salum Mvule, Magoti, Joseph Mwasenga, Hamis Shomar Gagarihno na Luku