Monday, 9 February 2015

TIMU YA FROLIDA YALAZIMISHA SARE YA 3-3 NA SURVEY VETERANS

Pamoja na kuchezesha vijana wadogo badala ya Veterans, Timu ya Frolida kutoka kimara ilijikuta ikilazimisha sare ya magoli 3-3 na Timu ngumu Tanzania bara na Visiwani Survey Veterans. Ikiwa ni mechi yake ya pili toka mwaka umeanza ikiwa imeshinda mechi moja na kutoka sare mara moja,  ilipambana vilivyo kuhakikisha haipotezi mchezo kirahisi na kulinda heshima yake katika uwanja wake wa nyumbani.

Timu ya Survey Veterans ipo katika maandalizi ya michuano ya Pasaka ambayo mwaka huu inafanyika Zanzibar kuanzia mwezi wa nne mwanzoni, inatarajia kuwa na mechi nyingi za kirafiki za ugenini ili kuzoea mazingira tofauti tofauti kwa ajili ya kujiandaa na michuano hiyo.

Picha zifuatazo hpo chini, ni za matukio ya mechi hiyo,,,

                                                                                                                        
   M/M/kiti wa SVSC full backleft Dr Rasul beki kitasa wa kutumainiwa baada ya kuisaidia timu     yake katika mechi na timu ya Florida Veterans
Mwl mkuu wa timu ya SVSC  Ramadhan Bomba akitoa maelekezo wakati wa mapumziko
            


    Peter Ngassa (Captain wa Svsc) kushoto na Shaban Kambabghe (K/Katibu wa Svsc) baada ya mpira kumalizika  Ngassa alikuwa golikipa siku ya mechi ambapo alichomoa michomo mingi sana siku hiyo....                                                           
 Mshambuliaji wa kutumainiwa wa Timu ya Survey  Richard. Mbunda baada ya kutolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Steven Nyenge
                 Beki nguli  Dr. Deusdedit Kibasa wa timu ya Survey Veterans baada ya mpira kumalizika...
                     Kiungo wa kutegemewa wa Svsc mtaala wa pasi za mwisho Steven Nyenge alitoa pasi mbili za mwisho na kuisaidia timu kupata mbao mawili

                          Said Sise  mshambuliaji hatari bada ya mpira kwisha anapoza koo.
                                    Captain msaidizi Ahmad Shaweji beki wa kati baada ya mpira kwisha

                         Bw. John Mbitu "mchezaji mwenye misuri minene" ambaye anawindwa na Rada za timu kubwa hapa mjini za VPL,,  mtaalam wa kukaa na mipira....

0 comments:

Post a Comment