Saturday, 9 August 2014

SVSC YALAZIMISHWA SARE NA KIKOSI B CHA TIMU YA COASTAL UNION YA JIJINI TANGA

Timu ya SVSC katika mechi yake ya pili jijini Tanga ililazimishwa sare na Mabingwa wa Uhai Cup kikosi cha pili cha Wagosi wa Kaya Costal Union katika uwanja wa Mkwakwani baada ya  kutoka sare ya bao 1-1 baada ya kuongoza kwa dk 70 za mchezo bao lililowekwa kimiani na mshambuliaji hatari Moses katika dak ya 27 kipindi cha kwanza. Dk 20 kabla mpira kumalizika vijana wa Costal union walisawazisha baada ya kutokea piga nikupige langoni mwa survey vetens.

PICHA MATUKIO YA MCHEZO HUO


Juu na chini ni kikosi kilichotoka sare na Mabingwa wa Uhai cup Timu B ya Costal Union 



 Picha chini Inamuonesha Capt Mohamed Adam "Zengwe" akionesha maufundi katika uwanja wa mkwakwani mjini tanga kabla mechi kuanza

 Picha juu kikosi cha Survey kikipasha misuli moto kwa ajili ya maandalizi ya mchezo....

Benchi la ufundi likiongozwa na Mwl Ramadhani Bomba likifuatilia mchezo kwa makini.....

0 comments:

Post a Comment