Timu ya SVSC katika mechi yake ya pili jijini Tanga ililazimishwa sare na Mabingwa wa Uhai Cup kikosi cha pili cha Wagosi wa Kaya Costal Union katika uwanja wa Mkwakwani baada ya kutoka sare ya bao 1-1 baada ya kuongoza kwa dk 70 za mchezo bao lililowekwa kimiani na mshambuliaji hatari Moses katika dak ya 27 kipindi cha kwanza. Dk 20 kabla mpira kumalizika vijana wa Costal union walisawazisha baada ya kutokea piga nikupige langoni mwa survey...