Thursday, 12 March 2015

TIMU YA NSSF VETERANS YALAZWA MABAO 2-1 NA SURVEY VETERANS

Timu ya NSSF Veterans ilijikuta ikitoka kwa huzuni katka Uwanja wa Chuo kikuu Ardhi baada ya kukubali kichapo cha magoli 2-1 kutoka kwa SVSC. Ilikuwa ni mchezaji ghali, mwenye pasi za macho, akitokea benchi, Steven Nyenye (Stevovo) aliyoipatia SVSC bao la ushindi baada ya kumalizia mpira uliotemwa na golikipa. Timu ya NSSF ikiongozwa na Dominic Mbwete ilionesha soka la kiufundi kuelekea mashindano ya NSSF ambayo yanatarajiwa kutimua vumbi katika...