Monday, 17 December 2018

MATUKIO KATIKA PICHA KABLA NA BAADA YA MCHEZO WA ULINZI VETERANS vs SVSC

Timu ya SVSC wakifanya mazoezi mepesi kabla ya mchezo kuanza. Captain Peter Ngasaa kushoto  wakijadiliana nani wa kuanza mpira katikati ni Dr. Tiboroa ambaye alikuwa refaree wa mchezo. Vidume vilivyoshereshea mchezo huo wakimsikiliza msemaji wa timu ya upinzani baada ya mchezo kumalizika. Ushindi raha....Baada ya ushindi wa mchezo wa leo. Bw. Frank Gaspar akijipongeza na Castle light baridiiii.... Duh........

ILIKUWA ZAMU YA ULINZI VETERANS

Kikosi cha Ulinzi veterans kabla ya mchezo kuanza Timu changa ya Ulinzi Veterans inayoundwa na maofsa wa jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania walijikuta katika wakati mgumu katika uwanja wao wa nyumbani Lugalo pale walipokubali kichapo cha magoli 2-0 kutoka timu kongwe ya Survey Veterans. Pasi mujarabu kutoka kwa Chacha Kibago ilimkuta winga hatari Musa Siwiti na kuukwamisha wavuni kutengeneza goli la kwanza na goli la pili lilifungwa na Albert...