Sunday, 19 July 2015

KATIKA KUSHEREHEKEA SIKUKUU YA EID PILI, BW, SHABANI K. ALIZALIWA

Tarehe 19/07/.... alizaliwa M/katibu wa Survey Veterans  Bw. Shaban K. katika siku ya sikukuu ya Eid pili ambapo M/kiti wa SVSC Bw, Peter Mweta aliungana na wanachama na wapenzi wa Survey Veterans katika kumpongeza Bw,Shabani katika siku yake ya kuzaliwa na kumtakia maisha marefu yenye amani na furaha tele.  Pia M/kiti alifungua shampagn isiyo na kilevi katika kumpongeza Bw, Shabani K. kwa kuzaliwa leo. Matukio ya picha yanaonesha mfululizo...

SURVEY VETERANS YAMPONGEZA MWANACHAMA WAO Dkt NGASAMIAKU KWA KUPATA Phd

M/kiti wa Survey Veterans Bw Peter Mweta aliungana na wanachama wa SVSC kumpongeza Dkt Ngasamiaku kwa kumaliza masomo yake na kupata Phd yake. Dkt Ngasamiaku ,alipopewa nafasi ya kusema chochote alisema', "Nawashukuru sana wapenzi na wanamichezo wa SVSC kwa maombi yenu ambayo naamini kwa njia moja ama nyingine yalifanikisha mimi kufikia hatua hii kubwa ya kielimu Mungu awabariki sana". Mwanachana na mchezaji wa SVSC Bw. Innocent Lyimo alifungua Champaign...

SURVEY VETERANS YASHEREHEKEA EID PILI KWA FURAHA

Kama ilivyo ada, kwa timu hii, kila mwaka husherekea kwa pamoja siku kuu ya Eid pili kwa matukio mbali mbali ikiwa ni njia mojawapo ya kukutana pamoja, kula pamoja na kufurahi pamoja. Sherehe ya mwaka huu inaweza ikawa imevunja rekodi kati ya sherehe kama hii zilizopita maana ilikuwa inaandaliwa kwa umakini na ueledi mkubwa chini ya Mhazini Mkuu Dkt R. Shukia (Sha-Makala). Wanachama pia walikuwa wengi ukilinganisha na miakailiyopita penhine kutokana...