Timu ya Survey Veterans kutoka Dar e salaam, imeilaza timu ya Mwanza StareheVeterans kwa magoli 4-2 katika uwanja wa CCM Kilumba Jijini Mwanza.Magoli ya Survey VeteransYalifungwa na Peter Ngasa, magoli 2,Innocent Lyimo na Said Omary kwa mkwaju wa penati.Magoli ya wenyeji yalifungwa na Juma Amir Maftah na Mbuyi Yondani. Kikosi kilichoizamisha Mwanza Starehe Veterans kiliongozwa na Golikipa Kilibe, fullbacks James Kabambo na Dr Rasul Ahmed, Center Backs Dr. Kibasa Na Kobi, Half Back six Mohamed Adam, Wingmidfielders Mzee Carlos na Shabani Kambabhe, Center forward Benson Hagai inside ten Peter Ngassa.
Kipindi cha pili yalifanyika mabadiliko, Mohamed Adam alitoka na Nafasi yake kuchukuliwa na Steven Nyenge, Benson Hagai akaingia David Kiganga, Carlos akaingia Said Omary, Dr Rasul akaingia Ahmad, Kabambo akaingia Kisanga , akatoka Innocent akaingia Edward Lila. Hadi mwisho wa mchezo Survey Veterans 4 na wenyeji Mwanza Starehe veterans2.]
mwal Bomba akitoa maelekezo baada ya mapumziko.... huku mzee carlos akiwa anapooza koo na maji baridi....
...Beki la kutumainiwa Dr D Kibasa akimsikiliza mwalimu kwa makini...
M/kiti na katibu wakitoa shukrani kwa wachezaji baada ya game kwisha na kushinda goli 4-2
...Baadhi ya wanachama wa SVSC wakifuatilia maelezo ya m/kiti kwa makini...
M/katibu Bw. Shabani Kambabheakiwa uwanja wa kirumba Mwanza kabla mchezo kuanza....
0 comments:
Post a Comment