Thursday, 5 April 2018

SALAMU ZA PASAKA KUTOKA MWENYEKITI WA SURVEY VETERANS SPORTS CLUB

Wadau habari za Jioni, wageni wetu kutoka Zanzibar waliondoka jana na kufika salama Unguja. Napenda kutoa shukurani za dhati kwenu nyote mlioshiriki na hata wale ambao hawajashiriki najua mlikuwa na nia ila mambo yaliingiliana. Kwa niaba ya kamati ya utendaji na ya wageni nasema ASANTENI SANA. Shukrani ziende kwa wale wote waliopewa majukumu na kuyatekeleza kikamilifu kabisa, Katibu, Mhazini,wapokeaji michango Mwalimu Bomba na Babu Carlos (wajela...

Tuesday, 3 April 2018

SURVEY VETERANS BINGWA WA HISTORIA MICHUANO YA PASAKA 2018

Captain wa timu ya SVSC Peter ngassa akinyanyua juu kombe la ubingwa wa Michuano ya Pasaka kwa mwaka 2018 baada ya kukabidhiwa na mgeni rasmi Mkurugenzi wa Ufundi TFF Mwl Salim Madadi aliyemwakilisha Naibu katibu mkuu wa TFF Bw. Wilfred Kidau. Pembeni ni Mwenyekiti wa SVSC Bw. Peter Mweta akishangilia kwa furaha. Mgeni Rasmi Mkurugenzi wa Ufundi TFF Bw. Salim Madadi akitoa maelezo mafupi kwenye ufungaji wa mashindano ya Pasaka kabla ya kutoa...

MICHUANO YA PASAKA: MECHI YA UTANGULIZI WAZEE SPORTS WAWAFUNGA WAZEE WA SURVEY VETERAN 2-1

   Kabla ya mechi ya fainali kulikuwa na mechi ya utangulizi iliyopigwa kati ya Wachezaji wenye umri zaidi ya miaka 50 kwa kila timu ambapo wazee Sports walishinda kwa magoli 2-1 John MBitu (Benteke) katika maandalizi ya mchezo wa utangulizi Kutoka kulia Dr. Rasul Ahmed, Pius na Bruce Herman wakipasha misuri moto kabla ya mchezo wa utangulizi ambazo SVSC ililala lwa mabao 2-1 ...

MICHUANO YA PASAKA: WAZEE SPORTS CLUB YATOKA SARE NA TANZANIA STARS

Timu ya Wazee Sports Club wakiwa wamechanganyika na wenyeji wao Survey Veterans wametoka sare ya kufungana magoli 2-2 na Timu ya Tanzania Stars ambayo inaundwa na wachezaji wa zamani wa timu ya taifa na vilabu vikubwa nchini Tanzania. Mchezo uliochezwa katika uwanja wa nyumbani wa Survey Veterans (OT) uliopo chuo kikuu Ardhi. Wachezaji wa Timu ya Tanzania Stars wakifanya mazoezi kabla ya mechi kuanza John Mbitu akiwa na kaka yake...