Tuesday, 15 October 2019

TANGA: MATUKIO YA NJE YA UWANJA

Pamoja na michezo ya Bonanza timu ilifurahi pamoja kama matukio ya picha yanavyoonesha... Madam Datah Daudi akiwaandalia chakula wachezaji baada ya mchezo kumalizika. ...

BONANZA TANGA: ARUSHA ALL STAR YALALA KWA 3-1 MBELE YA SURVEY VETERANS

Mchezo wa pili dhidi ya Arusha All Star walikubali kichapo cha magoli 3-1 Magoli yaifungwa na Kelvin, Ngasa na Sisse. Nahodha wa Survey Veterans Peter Ngassa akimiliki mpira na mchezaji wa Arusha all Star akifuatia kwa karibu.. Arusha ililala kwa magoli 3-1. ...

BONANZA TANGA: SVSC YALAZWA 2-1 NA KOROGWE VETERABS

Mvua kubwa....Hivi ndivyo ilivyokuwa... Kiungo hatari na Naodha wa timu ya SVSC Peter Ngassa akimsaidia Kelvin Haule mwenye  mpira katika mechi ilikuwa iichezwa kwenye uwanja uliojaa maji. Mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha mkoani Tanga ilisababisha uwanja kuwa katika hali mbaya na kupelekea SVSC kufungwa magoli 2-1 kwa Tabu sanaaaa Kelvin haule  Mwenye jezi namba 31 wa SVSC akiwa amekusanya kijiji kuelekea golini kwao ....Gooooooool....

SURVEY VETERANS ZIARANI TANGA

Timu ya SVSC imeondoka leo kuelekea jijini Tanga. Pamoja na mambo mengine itashiriki Bonanza liliandaliwa na Timu Mwenyeji ambapo timu kama Moro Veterans, Tanga Veterans ,Kitambi noma Veterans na Timu zingine zinashiriki katika bonanza hilo. ...

SURVEY VETERANS YALALA 2-0 MBELE YA TPDC

Winga hatari Musa Siwiti akiwindwa na mabeki watatu wa timu ya TPDC katia mchezo uliofanyika katika uwanja wa TPDC . Ikichezesha vijana badala ya Veterans Timu ngumu ya SVSC ilifungwa wa tabu na timu ya TPDC. Ilibidi wasubiri hadi kipindi cha pili kupata magoli baada ya mchezo mzuri uliooneshwa na SVSC. Sha- Pelle akiwa katika kumiliki mpira mbele ya mabeki wawili wa TPDC  katika mchezo ambapo SVSC ililala kwa 2-0 Revis akimiliki...