
Zikicheza katika uwanja mdogo wa Taifa (Shamba la Bibi) timu ya Twalipo Veterans ilijikuta katika wakati mgumu baada ya kuongoza kwa magoli 4-0 hadi kipindi cha kwanza kumalizika. Timu zote zilifanya mabadiliko na timu ya SVSC mabadiliko yake yalionekana kuwa na manufaa zaidi pale walipopata magoli mawili ya haraka ambapo goli la kwanza lilifungwa kwa mkwaju wa penati na Peter Mweta baada ya Paschal Fumbuka kufanyiwa madhami katika eneo...