
Timu ya Lugaro veterans iliendelea kuwa wateja wa Survey Veterans kwa mwaka wa tatu mfululizo baada ya kukubali kipigo kingine cha mabao 2-1. Ilikuwa Lugaro veteran iliyoanza kujipatia goli la kuongoza katika kipindi cha kwanza, lakini iliwachukua dk 20 tu SVSC kusawazisha kupitia winga wake hatari Dula.
Hadi timu zinaenda mapumziko zilikuwa zimefungana magoli 1-1.
Akitokea bench mshambuliaji hatari wa SVSC Said Sisse aliipatia SVSC goli la kuongoza...