Ndugu wana michezo, ni mwendelezo wa matukio ya kumuaga ndugu yetu Bw. Bruce Heilman ambaye anamaliza muda wake wa kukaa Tanzania. Picha zifuatazo zinaonesha matukio.
Picha chini... inamuonesha Mwenyekiti wa SVSC Bw. Peter Mweta akimkabidhi Bw. Bruce Heilman kikombe chenye nembo ya timu ya SVSC kama mojawapo ya zawadi huku Katibu mkuu Bw. Suleiman akishuhudia kwa karibu.

M/M/kiti Bw. Rasul Ahmed alimkabidhi Bw. Bruce Helmain Kinyago chenye nembo ya timu ya SVSC kama moja ya zawadi alizokabidhiwa...
Mwenyekiti akionesha kikombe chenye nembo ya timu kikiwa kimeandaliwa na uongozi wa SVSC kama mradi wa kutunisha mfuko wa timu. Vikombe vipo kwa mwanachama na wapenzi watakao hitaji. Gharama yake ni tsh. 18,000/= tu.
....Hiki chakula ni kitamuu!!!!! Bw. B Magadula akimweleza Joseph wakati wakipata msosi
...".Ongeza ongeza.... hii biriani tamu sana"
Mwisho Bw. Bruce aliwashukuru wanachama na wachezaji wenzake ( hawapo pichani) kwa moyo wao wa upendo. na kuwatakia maisha mema na yenye furaha. Mungu akupenda tutaonana tena alimalizia.....
0 comments:
Post a Comment