
Mapinga Veterans walijikuta katika wakati mgumu pale walipokubali kipigo cha magoli 4-1 mbele ya Timu ngumu ya Survey Veterans katika uwanja wa chuo kikuu Ardhi. Iliwachukua dk 15 timu ya SVSC kupata magoli mawili ya kuongoza kufuatia pasi nzuri za winga wake hatari Musa Siwiti ambazo zilimfikia Dulla na kuzikwamisha wavuni. Hadi mpira unamalizika SVSC 4 na Mapinga Veterans bao 1.
...