Timu ya Lugaro veterans iliendelea kuwa wateja wa Survey Veterans kwa mwaka wa tatu mfululizo baada ya kukubali kipigo kingine cha mabao 2-1. Ilikuwa Lugaro veteran iliyoanza kujipatia goli la kuongoza katika kipindi cha kwanza, lakini iliwachukua dk 20 tu SVSC kusawazisha kupitia winga wake hatari Dula.
Hadi timu zinaenda mapumziko zilikuwa zimefungana magoli 1-1.
Akitokea bench mshambuliaji hatari wa SVSC Said Sisse aliipatia SVSC goli la kuongoza ambalo lilidumu hadi mwisho wa mchezo baada yakumpiga chenga beki wa mwisho na kumchugulia golikipa na kuupeleka mpira upande wa kushoto na kumuacha golikipa akiruka kulia bila mafanikio.
 |
"leo hawapati hata bao moja" Golikipa namba moja wa SVSC Kilibe jumbe anamwambia M/kiti Peter Mweta dk chache kabla ya mechi kuanza. |
 |
"Mwl. R. Bomba akitaja kikosi kitakachoanza " hawapo pichani |
 |
"Mabeki visiki " Kushoto ni Joseph Mwasenga na kulia ni M?M?kiti Dr. Rasul Ahmed wakimsikiliza mwalimu kwa makini. |
 |
"Mtaalamu wa mipira ya vichwa" Said Seif", David kiganga na Winga machachari Jumanne wakimsikiliza mwalimu |
 |
M/Katibu Bw. Shabani Kambabhe mbele mwenye soksi nyeupe, Bw. Hassan na said seif wakimsikiliza mwalimu kwa makini |
 |
Beki hatari asiyepitika kirahisi Dr. D Kibasa, ni beki inayotajwa kuwa clean sheet nyingi ukilinganisha na mabeki wengine" wa SVSC |
 |
"Eeh Mwenyezi Mungu tunaomba utujaalie tushinde mechi hii". Hivi ndiyo anavyosema golikipa hatari wa SVSC |
 |
"Winga teleza"Musa Siwiti winga mwenye mbio sana na mpishi mzuri wa magoli akijiandaa kuanza mpira. |
0 comments:
Post a Comment