Thursday, 12 March 2015

TIMU YA NSSF VETERANS YALAZWA MABAO 2-1 NA SURVEY VETERANS

Timu ya NSSF Veterans ilijikuta ikitoka kwa huzuni katka Uwanja wa Chuo kikuu Ardhi baada ya kukubali kichapo cha magoli 2-1 kutoka kwa SVSC. Ilikuwa ni mchezaji ghali, mwenye pasi za macho, akitokea benchi, Steven Nyenye (Stevovo) aliyoipatia SVSC bao la ushindi baada ya kumalizia mpira uliotemwa na golikipa. Timu ya NSSF ikiongozwa na Dominic Mbwete ilionesha soka la kiufundi kuelekea mashindano ya NSSF ambayo yanatarajiwa kutimua vumbi katika siku chache zijazo.

Baadhi ya Kikosi kilichopeleka kilio kwa NSSF Veterans. Kutoka kulia ni Musa Siwiti, Benson Hagai, David Kiganga,James Kiganga, Joseph Mwasenga, John MBitu na Elirehema Kisanga golikipa hatari Kilibe Jumbe



(Kuelekea mechi ya watani wa jadi Simba na Yanga) Innocent Lyimo akionesha "Hii soksi ya ushindi japo tumevaa jezi nyekundu"

 Baadhi ya wachezaji walioshiriki katika mchezo wa kirafiki kati ya SVSC Veterens na NSSF Veterans. kutoka kushoto ni straika hatari Hassan,Innocent Lyimo wa mbele soksi za njano, Carlos Milinda (babu), James Kabambo,Kilibe Jumbe, Shaban Kambabhe, Musa Siwiti, Aman Simba, Capt  Mohamed Adam. Na waliosimama mstari wa nyuma ni Benson Hagai, Joseph Mwasenga,John Mbitu na Elirehema Kissanga

0 comments:

Post a Comment