Wednesday, 1 January 2020

TIMU MAGIGE YALALA MBELE YA TEAM DETAH

Timu Manager Madam Detah akiwa na Captain wake Mohamed Zengwe kabla ya mchezo kuanza.

Kama ilivyo kawaida kwa Timu ya Survey Veterans kusherehekea Siku kuu ya mwaka mpya kwa kucheza mechi za Wenyewe kwa wenyewe.  Timu Ziliundwa kwa kusaidia na Manahodha wa pande zote mbili Timu zilipewa majina ya wanachama Wenzetu ambao ni wanawake Dada Datah na Mama ambaye hutuhudumia juice wakati wa Mazoezi. Baada ya mpambano mkali timu ya Detah ilishinda goli 1-0 lililofungwa na Iddi Kaoneka (Mnyama ) kwa kwa njia ya penati baada ya Sise kufanyiwa madhambi kwenye eneo la hatari.
Kikosi Ushindi: kutoka kulia waliosimama Sahid Mahoka, Ahmad Shaweji, Momo, Shabani Kambabhe, Peter Mweta, Team Manager Madam Detah. Walioinama kutoka kulia ni Kelvin,Michael ,Makoye, Musa siwiti,Shevy,n Golikip Mwandumbya. Waliokaa chini ni Peter Ndosa na Mohamed Adam.

Timu Magigi waliosimama kutoka kushoto ni Team Manager Madam Magigi, Bilauri, Osca Kobby, Mwenyekiti John Mbitu, Peter Simon, Nyigu, Wiliam Golikipa, na waliochuchumaa ni Mzee ndugulu kushoto, Batton, Salum Mvule, Magoti, Joseph Mwasenga, Hamis Shomar Gagarihno na Luku












0 comments:

Post a Comment