Mashindano ya Shirikisho la Mashirika ya umma na Makampuni binafsi Tanzania ( SHIMMUTA)yalimalizika tarehe 30/11/2014 mkoani Tanga kwa timu ya Mikopo kuchukua ubingwa wa Mpira wa miguu, Timu ya TBCkutwaa bingwa wa Mpira wa pete na Chuo kikuu ardhi kutwaa ubingwa wa mpira wa kikapu
Baadhi ya wanachama na wachezaji wa SVSC walishiriki mashindano hayo kutokea katika taasisi zao wanazofanyia kazi.
Majina ya Wachezaji wa SVSC walioshiriki (SHIMMUTA) na taasisi/makampuni wanakofanyia kazi. kwenye mabano Frank Gaspar, Musa Siwiti, Dr. Kibasa, Benson Mwemezi, Joseph Mwasenga (Chuo kikuu Ardhi), Ahmed Salum, Shukuru. Hale Temba (TBC), Ramadhani Bomba, Dr.Rasul Ahmed, Dr Shukia Richard, Richard Mbunda ,Faraji na Oliva Katanje (UDSM). Mashindano yalikuwa mazuri na ya ushindani. Pia taasisi nyingi zilishiriki japo zingine hazikuleta timu zao.
Monday, 1 December 2014
MASHINDANO YA SHIMMUTA TANGA 2014 YAMALIZIKA
21:42
No comments
0 comments:
Post a Comment