Katika kuukaribisha mwaka mpya kumekuwepo na matukio ya kufurahisha na mwanzo mzuri kwa ushirikiano baina ya wachezaji na wanachama.
Kumekuwepo na hali ya ushindani katika mazoezi ambapo, baadhi ya wanachama wenzetu Bw. James Kabambo, Bw, Richard Shukia na Bw John Mbitu walitoa zawadi ambazo zilishindaniwa na timu ambazo mwalimu amekuwa akiziteua wakati wa mazoezi. Ambapo katika mechi ya jumapili Bw Carlos alifunga magoli matatu peke yake (hart-trick) na kukabidhiwa mpira.
Hali hii imeongeza hari na ushindani katika mazoezi, pia kumekuwepo na ongezeko kubwa la wanamichezo na wanachama kuja kuangalia mazoezi.
Pia timu ilipata wanachama wawili wapya ambao ni Bw. George Nshunju na Bw. Stephen Kayan ambao walipewa form na kujaza na kuzirudisha kwa uongozi.
Matukio ya picha yanaonesha ....
Monday, 5 January 2015
MATUKIO KATIKA KUUKARIBISHA MWAKA MPYA 2015
00:08
No comments
0 comments:
Post a Comment