Friday, 3 April 2015

TIMU YA SURVEY VETERANS YALAZIMISHWA SARE NA TIMU YA KOMBAINI YA VETERANS YA ZANZIBAR





Ilikuwa penati iliyopigwa kwa ufundi mkubwa na Katibu mkuu wa SVSC Bw, Suleiman Mgaya iliipatia timu ya Survey  Veterans goli la kuongoza katika kipindi cha kwanza katika mechi iliyochezwa usiku katika uwanja wa Amani mjini Zanzibar baada ya Mshambuliaji mwenye misuri minene kuangushwa katika eneo la hatari na mwamuzi kuamua ipigwe penati

Kipindi cha pili kilianza kwa kila timu ikifanya mabadiliko mbalimbali ambapo Timu ya kombaini ilipata goli la kusawazisha, lakini timu ya SVSC inabidi ijilaumu yenyewe baada ya kukosa mabao matatu ya wazi baada ya straika wake hatari Richard Mbunga akiwa yeye na golikipa wa kombaini aligongesha mwamba wa juu na mpira kumkuta Edwin Mfanga ambaye naye aligongesha mwamba na mpira kutoka nje.

Katika harakati za kuokoa mpriga Beki hatari wa kutumainiwa wa SVSC , Ahmed Salumu aligongana na golikipa wake na mshambuliaji wa timu ya Kombaini na kumuumiza puani na kukimbizwa hospitali baada ya hali yake kuwa siyo nzuri. Hadi kipenga cha mwisho kinapulizwa na mwamuzi aliyeinyima penati ya wazi timu ya SVSC magoli yalikuwa sare ya goli 1-1

0 comments:

Post a Comment