Friday, 3 April 2015

TIMU YA SURVEY VETERANS SPORTS CLUB ZIARANI ZANZIBAR KWA AJILI YA MICHEZO YA PASAKA



Timu ya SVSC imeondoka leo jijini Dar es salaam kwa boti ya Kilimanjaro kwenda Zanzibar kwa ajili ya michezo ya Pasaka. Timu imewasili salama visiwani humo na kupokelewa na wenyeji wao Wazee Veterans ya Visiwani humo.Timu imeondoka na wachezaji 23 na viongozi 4 ambao ni Bw. Suleiman Mgaya (Katibu Mkuu Mkuu wa msafara) Richard Shukia ( Mhazini mkuu), Ramadhani Bomba Mwalimu wa timu na Benson Mwemezi M/Mhazini.

Wachezaji walioongozana na timu ni pamoja na Golikipa hatari Kilibe Jumbe,Athuman Kione, Pius Joseph, Mohamed adam (M/kiti wa Mashindano, Josephat Edmund, Faraji Ghalib,Peter Ngasa (Captain), Steven Nyenge, Beki hatari Osca Mwambinga. Wengine ni Frank Gaspar, (mjumbe kamati ya nidhamu) Said Mahoka, Enock James, Ally Mgaya (mjumbe kamati ya ufundi), David Kiganga,Said Omary,Musa Siwiti (mjumbe kamati ya nidhamu (blogger), Ahmed Salum, Richard Mbunda na Macocha Tembele.
Timu ikiwa visiwani humo, itashiriki michezo ya Soka, kuvuta kamba pamoja na Pool table. Timu inatarajia kurejea jijini Daresalaam tarehe 3/4/2015 na ushindi wa michezo yote iliyotajwa hapo juu baada ya kufanya mazoezi ya kutosha.

0 comments:

Post a Comment