Wednesday, 8 July 2015

TIMU YA MBEZI VETERANS YALALA 2-1 DHIDI YA SURVEY VETERANS


Iliwachukua dk 23 tmu ya mbezi veteran inayochezewa na mchezaji ambaye ni mwanachama wa Survey veteran Bw Octor kupata goli la kuongoza lililofungwa kwa mkwaju mkali kutokea upande wa kushoto. Kabla ya kwenda mapumziko Timu ya survey ilisawazisha kupitia kwa winga wake hatari Moses baada ya kupokea pasi mujarab kutoka kwa Peter Mweta (Mwenyekiti).

Kama ilivyo ada kwa Survey Veterans kucheza kwa dk 120 waliweza kupata goli la kuongoza liliofungwa tena na Moses. Kila timu ilifanya mabadiliko kadhaa ila matokeo yalibaki kwa survey Veteran kushinda mchezo huo.





0 comments:

Post a Comment