Wednesday, 4 May 2016

MAADHIMIO YA MKUTANO MAALUM WA WANACHAMA NA WAPENZI WA SURVEY VETERANS SPORTS CLUB

MAADHIMIO YA MKUTANO  MAALUM WA WANACHAMA NA WAPENZI WA SURVEY VETERANS SPORTS CLUB

Ndugu wanachama na wapenzi wa SVSC napenda nichukue nafasi hii kuwafahamisha kuwa, kufuatia mkutano mkuu wa kawaida wa wanachama uliofanyika tarehe 26/o4/2016, yafuatayo yaliamuliwa.

  1. Ada ya uanachama itabali ileile ya Tsh 10,000/= kwa mwezi.
  2. Wale wote ambao walihuisha uanachama wao na wanachama wapya ambao walikuwa na madeni ya ada waanze kulipa madeni yao kuanzia mwezi wa tano (May) ili kuendelea na uanachama, vinginevyo itakapofika mwezi wa sita June) uanachama wao utakoma.
  3. Kundi la mawasiliano la SVSC litatumika kwa wanachama tu. Hivyo, kuanzia jumapili ijayo tarehe 09/05/2015 wale wote ambao si wanachama WATAONDOLEWA.
  4. Wanachama watapewa kipaumbele katika maswala yote yanayohusiana na klabu kuanzia kucheza uwanjani,safari n.k
  5. Wachezaji wasio wanachama wataendelea kucheza kama kawaida na hawatakuwa wakichangia chochote katika timu.
  6. Hakutakuwa na utaratibu wa mchango wowote kwa asiye mwanachama kuhusiana na masuala mbalimbali ya kijamii.
  7. Mkutano ulimchagua Ndugu Bluce Heilman kuwa mjumbe wa kamati ya utendaji kuziba nafasi iliyoachwa wazi na na aliyekuwa mjumbe kwa wakati huo Ndugu Salvatory Malongo.
MWISHO:
Natoa rai kwa wale wote ambao hawajaamua kuwa wanachama wa SVSC wafanye hivyo ili kuendeleza umoja na udugu tunaoendelea nao bila kumuacha yeyote nyuma kwa faida yetu wote wana SVSC.
MUNGU IBARIKI SVSC IDUMU.

Peter Mweta
Mwenyekiti


0 comments:

Post a Comment