SURVEY VETERANS SPORTS CLUB YAFANYA ZIARA YA KIMICHEZO JIJINI MBEYA
 |
Kikosi kamili kilichowakilisha Mbeya kutoka kulia walioinama, Osca Mwambungu,Mohamed Adam (Captain) Ahmed Shaweji,Suleiman Mgaya,Innocent Lyimo na Benson Hagai. kutoka kushoto waliosimama, Dkt Rasul Ahmed,Arbet Sengo,Steven Nyenge,Peter Mweta na Ramadhan Bomba (Mwalimu wa Timu) |
Timu ya mpira wa miguu ya Survey Veterans Sports Club imefanya ziara ya michezo ya kirafiki jijini Mbeya baada ya kupokea mwaliko kutoka timu Mwenyeji ya Mbeya Veterans. Timu iliondoka jijini Dar esa laam kwa Ndege ya Fastjet siku ya ijumaa ikiongozwa na Mwenyekiti Peter Mweta, M/M/kiti Dkt Rasul Ahmed, Katibu Mkuu Suleimani Mgaya, K/Katibu Shabani Seleman, Mwalimu wa Timu Ramadhani Bomba Capt Mohamed Zengwe na wengine. Timu ilifika salama jijini Mbeya na kupokelewa na wenyeji na kupelekwa hotelini.Timu ilicheza michezo miwili ya kirafiki na timu B ya Mbeya City na kufungwa magoli 2-1. na Mchezo wa pili ilicheza na wenyeji wao Mbeya Veterans na kutoka sare ya goli moja kwa moja Timu ilikaa jijini mbeya kwa siku mbili na kurejea Dar es salaam siku ya jumapili tarehe 29/05/2016
MATUKIO YA PICHA KATIKA ZIARA HIYO
 |
Arbart Sengo kutoka kushoto, Innocent Lyimo na Benson Hagai golikipa katika maandalizi ya mwisho kabla ya mchezo |


Katibu Suleiman Mgaya kushoto na Innocent lyimo kulia kabla ya mchezo


Dkt Rasul Mwalimu wa timu na Golikipa hatari katika maandalizi ya mwisho kabla ya mchezo
 |
Mbwiga wa Mbwiguke alikuwa mchezaji mwalikwa katika timu ya SVSC katika mchezo wa kwanza |
Safi sanaaa!
ReplyDelete