Saturday, 13 August 2016

NSSF VETERANS YAPIGWA GOLI 2-1 NA SURVEY VETERANS KATIKA UWANJA WA JK PARK

Timu ngumu mkoa wa  Dar es salaam Survey veterans  jana ilipeleka kilio tena kwa wenzao wa NSSF Veterans walipojaribu kujiuliza tena baada ya mechi ya awali kutoka sare na SVSC kwa kuwafunga bao 2-1. Pasi nzuri kutoka kwa foward hatari Benson Mwemezi ilimfikia Winga hatari Musa Siwiti na kuukwamisha mpira wavuni na kuandika bao la kuongoza katika dakika 15 ya kipindi cha kwanza.
Pia winga hatari Musa Siwiti nusura aipatie SVSC bao la pili pale shuti lake kali lilipogonga mwamba na kutoka nje baada ya kona nzuri iliyochongwa na James Kabambo. Hadi timu zinaenda mapumziko SVSC ilikuwa inaongoza kwa goli 1-0.
Kipindi cha pili kilianza baada ya kila timu kufanya mabadiliko na SVSC walifanikiwa kupata goli la pili lililofungwa na Humprey Machota baada ya kuwashinda nguvu walinzi wa NSSF Veterans na kuukwamisha mpira wavuni. Dakika 10 kabla ya mpira kumalizika NSSF walipata bao la kufutia machozi kupitia winga wao hatari baada ya kumalizia mpira uliotemwa na golikipa wa SVSC. Mpira ulianza saa mbili usiku na kumalizika saa tatu na nusu usiku.

Na Blogger wako.....  Sha_makala

Uwanja wa JK Park unavyoonekana wakati wa usiku ambapo timu ya NSSF ilipomenyana na tina ngumu mkoa wa Dar esa salaam Survey Veterans na kukubali kibano cha bao 2-1

Mchezaji Mwenyeji Dominic Mbwete mwenye jezi ya njano, akiteta jambo na washabiki wa Survey Veterans kabla ya mchezo kuanza ambapo Timu yake ililala kwa bao 2-1



0 comments:

Post a Comment