Saturday, 13 August 2016

TIMU YA SURVEY VETERANS YASHINDA GOLI 2-1 MICHUANO YA 88 MKOANI MOROGORO

Mchanganyiko wa Timu ya SVSC na Reli Veterans kabla ya mchezo kuanza

Timu ya Survey Veterans ilifanya ziara ya kimichezo mkoani Morogoro na kucheza mechi ya kirafiki na Timu ya Reli Veterans ya Morogoro na kuifunga goli 2.-1. Hadi timu zinaenda mapumziko Timu ya Reli Veterans ilikuwa inaongoza kwa goli 1-0. Goli la kusawazisha lilifungwa na Godwin ekingo na goli la pili na la ushindi lilifungwa na Captain Peter Ngassa baada ya kuiadaa ngome ya wapinzani na kufunga goli la kusawazisha.
LISTI YA WACHEZAJI WALIOILETEA USHINDI TIMU YA SURVEY VETERANS

  1. Shah (Golikipa)
  2. Innocent Lyimo
  3. Salum Mvule/Mbwete Dominic HT
  4. Charles Antipas
  5. Hamad Shaweji
  6. Mweta Peter/Dulaa (Dk 32 maumivu ya paja)
  7. Frank/Kiganga Dk 56
  8. Ngassa Peter (Capt)
  9. Ekingo
  10. Suleiman Mgaya
  11. Japhet/Momo Cisse
SUB ZINGINE
Suleima Mgaya /Koba
Mwl Ramadhan Bomba akitoa maelekezo ya mwisho kabla ya mchezo, Kutoka kulia Dominic Mbwete,Godwin Ekingo, Suleiman Mgaya (katibu),Charles Antpas, Capt Peter Ngasa,Innocent Lyimo, Sisse Momo, David Kiganga Dulla na Peter Ngasa
Timu zote mbili zikisalimiana kabla ya mchezo kuanza



"Wanaongoza, Siyo mbaya ndiyo mchezo, ila bado nafasi tunayo tukitulia...." Maneno ya mwalimu Ramadhani Bomba baada ya kipindi cha kwanza kumalizika na Reli Veterans walikuwa wanaongoza kwa goli 1-0

Dah... Game "tight" ndiyo inanyooneka wachezaji wakijadili Frank Gasper mwenye raba, Charles aliyevua jezi, Ekingo anayevaa kiatu waliosimama Peter Ngassa ,David Kiganga na Suleimani Mgaya na wengine katika kipindi cha mapumziko

0 comments:

Post a Comment