Friday, 14 April 2017

SURVEY VETERANS YASAFIRI LEO KWENDA ZANZIBAR KWA MICHEZO YA PASAKA


Wadau, kwa niaba ya uongozi wa SVSC na jamii yake yote napenda niwataarifu team itasafiri kwenza Zanzibar kama ilivyopangwa siku ya Ijumaa tarehe 14th April na kurudi J3 17th April. Wanaosafiri nawafahamisha kuwa reporting time saa 12:30 asubuhi na Chombo kinaondoka saa 1:00 kamili asubuhi hayo ni masaa ya kiswahili. Tickets zipo kwa Katibu na yeye ndio mratibu na mkuu wa msafara. Napenda kutoa shukrani mno kwa wale waliochanga na wakashindwa kusafiri ila wakatoa nafasi zao kwa wenzetu, pia na wale ambao wametusaidia kutupatia ya maji bila wao kusafiri na vile vile ambao wameshindwa kabisa tunaamini si kwa matakwa yenu. Wale waliotuahidi bado tunapokea, wale ambao hawajakamilisha naomba muwasiliane na Katibu moja kwa moja maana Katibu kaazima mahali kuogopa kuchelewa ili tusikose tiketi. Asanteni sana kwa ushirikiano huu, tuombeane safari njema na michezo mema tuendeleze ushindi tuliopata mwaka jana hapa kwetu DSM.

Wasalaam,
Peter Mweta
 Mwenyekiti

0 comments:

Post a Comment