Mechi ya pili tulicheza na Wenyeji Neighbours Veterans na kuwafunga goli moja liliwekwa kimiani na Chacha Kibago. Mechi ya tatu SVSC ilishinda kwa magoli mawili magoli yote yakifungwa na Albert Sengo kwa kumalizia shuti kali la Musa Siwiti ambalo golikipa alilitema.
Mchezo kwa ujumla ulikuwa mzuri na timu ilicheza kwa uwelewano mkubwa sana. Pia timu ya SVSC ilitoa washindi wawili kwenye mbio za mita 100. Innocent Lyimo akichukua zawadi ya Ushindi wa kwanza na Joseph Mwasenga akichukua ushindi wa tatu.
![]() |
Innocent Lyimo aliyevua shati akipokea zawadi yake ya mshindi wa kwanza wa mbio za mita 100 baada ya kuibuka mshindi kati ya washiriki 8 walioshiriki mbio hizo |
Pia Golikipa namba moja Sha_Pelle alichukua golikipa bora wa mechi ya kwanza na Hamisi Gaga alichukua uchezaji bora mechi ya kwanza
0 comments:
Post a Comment