Heri ya mwaka mpya 2018 wana Survey Veterans Sports Club.
Mwaka 2017 tumeshauacha na changamoto zake la msingi ni
kumshukuru Mungu Kwa uzima na afya njema alizotuzawadia hadi tunaweza fika na
kufanya mazoezi/mechi pamoja na kutekeleza majukumu yetu ya kila siku.
Ki timu changamoto kubwa zilizojitokeza ni,
1) Kumekuwa na ongezeko la matokeo mabaya katika mechi
tulizocheza kulinganisha na kipindi cha nyuma naomba Benchi zima la ufundi
iliangalie hilo.
2) Kupitia uongozi kumekuwa na mapungufu sana ya ukusanyaji
wa Ada za mwezi hili tutalirekebisha kuanzia kwetu sisi uongozi ili Mambo
yaendelee vizuri.
Mwaka 2017 tumekuwa na mazuri mengi sana hasa kimechezo
mbali mbali ya ndani na nje ya Dar, hatukukwama kusafiri,au kushiriki lolote
lililokuwa linatupasa kushiriki, hatujakwama kujitunza Kwa maana ya vifaa pia
na kusaidiana katika matatizo/mafanikio mbali mbali.
Katika hayo nawashukuru sana Kwa niaba ya Uongozi.
Vile vile nawapa pole sana wale waliopata misiba na matatizo
mbali mbali sambamba na hilo nawapongeza wale wote waliofunga ndoa na waliopata
mafanikio binafsi katika upambanaji wa kimaisha. PhD holders wanaongezeka sana.
👏🏾👏🏾👏🏾
2018 iko mbele yetu,Wazanzibari wanakuja pamoja na mengineyo
naendelea kuwaomba ushirikiano wenu.
Mungu ibariki Tanzania.
Mungu ibariki SVSC.
Mwenyekiti SVSC.
0 comments:
Post a Comment