Katika uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 9/2/2019 wanachama na wapenzi wa SVSC walimchagua Bw. John Muriu Mbitu kuwa Mwenyekiti mpya kwa kura 24 za ndiyo kwa kipindi cha miaka minne (4).Bw. Mbitu alimshinda Bw Peter Mweta ambaye alikuwa anagombea kwa mara ya pili kwa kupata kura saba (7).Viongozi wengine waliochaguliwa ni.Eng. Shaban Kambabhe Makamu Mwenyekiti
na Bw Suleiman Rajab Mgaya kuwa Katibu Mkuu
Nafasi ya Mhazini mkuu haikupata mgombea kwa hiyo uchaguzi mdogo utafanyika baada ya uongozi mpya kuingia madarakani ili kujaza nafasi hiyo.
Pia Mkutano mkuu uliwachagua wajumbe wa kamati kuu tendaji kama ifuatavyo
1. Peter Simon
2. Benson Mwemezi Hagai
3. T. Bilauri
4. Joseph Shauritanga
wajumbe wengine wawili Bw. Ally Mgaya na Bruce Helman kura zao zililingana na kuamuliwa kwamba utaitishwa uchaguzi mdogo ili kujaza nafasi ya mjumbe mmoja.
0 comments:
Post a Comment