Tuesday, 26 August 2014

MECHI YA KIRAFIKI KATI YA SVSC NA AZAM VETERANS

Ndugu wanamichezo na wapenzi wa SVSC, Kutakuwa na mechi ya kirafiki kati ya Timu yetu na Timu ya Azam Veterans  siku ya ijumaa tarehe 29/08/2014 saa 11:30 jioni katika uwanja wa Azam Complex Chamazi.
Kwa kuwa itakuwa ni siku ya kazi, tunashauriwa kuwasiliana ili kusaidiana usafiri kwa wale wenye vyombo binafsi vya usafiri ili tuweze kuwahi kufika kwa pamoja. Naomba tusaidiane kwa hili ili kuweza kulinda heshima hii tuliyopewa na wenzetu wa Azam.

Nawatakia Utekelezaji Mwema.

Suleiman Mgaya
Katibu Mkuu 
SVSC

0 comments:

Post a Comment