Mkurugenzi mtendaji wa Etina bar & Restaurant Bi Catherine Swai amewapongeza wapenzi na wachezaji wa timu ya Survey Veterans kwa ushindi wao walioupata katika Bonanza la Serengeti fiesta lililofanyika katika viwanja vya TCC Sigara Chang'ombe. Pia Mwenyekiti wa SVSC Bw. Peter Mweta alimshukuru kwa kutambua mchango wao katika kulitangaza jina la Bar hiyo.
Mwenyekiti Bw. Peter Mweta aliwaongoza wachezaji na wanachama katika zoezi la kukata keki kama matukio ya picha yanavyoonesha....

Mkurugenzi wa Etina Bar & Restaurant Bi Catherine Swai akiwa katika picha ya pamoja na Kipa mkongwe Bw. Peter Poka, Bw. Innocent na Bw, Musa Siwiti katika sherehe hiyo....
" Hii mishkat kiwango" Bw. Omar bawaziri akifurahia mshikaki huku Bw. Kilibe naye akijilamba kwa utamu.....
Bw. akifungua Champagne kuashiria ufunguzi wa sherehe hiyo...
" Isee tamu" mwasenga anawaambia wanachama na wapenzi wa SVSC
Bw. Omar Bawazil na Bw. Joseph Mwasenga wakiteta jambo siku ya sherehe
" Kukata keki raha" Hivyo ndivyo inavyoeleka kusema Mwenyekiti Bw. Peter Mweta akikata keki nyuma yake Captain Bw. Peter Ngasa, Bw. Steven Nyenge ,Blogger Bw Musa Siwiti na Mjumbe kamati ya ufundi Bw. Ally Mgaya wakishuhudia kwa karibu kabisa.
Sherehe iliambata na kinywaji kama ambavyo Mwl Bw. Ramadhani Bomba akipata mvinyo akishereekea ushindi
0 comments:
Post a Comment