Sunday, 15 March 2015

TIMU YA VIJANA YA KIBANGU YAIFUNGA TIMU YA WAZEE WA SURVEY VETERANS MAGOLI 7-3

Katika maandalizi yake ya kwenda Zanzibar kushiriki Bonanza la Pasaka, Timu ya SVSC iliialika timu ya Vijana ya Kibangu ambayo ina wachezaji wengi wanaochezea timu mbali mbali za ligi daraja la kwanza na la pili Taifa, ili kujipima nguvu na kuona kama inaweza kuhimili mikikimikiki ya Bonanza ambapo baadhi ya timu huko Zanzibar huchezesha vijana. Iliwachukua dk 10 tu vijana wa Kibangu kupata bao la kuongozabada ya mabeki wa timu ya SVSC kuzembea. Timu ya Wazee wa Survey ambayo jana ilikuwa haina golikipa wake hatari, ambaye alikuwa anauguliwa, golini alikaa Capt Peter Ngasa ambaye siyo mzoefu kukaa golini ndiyo maana ilikuwa rahisi kwa wapinzani "kujilia pweza gizani" Krosi safi iliyochongwa na winga hatari, winga wa kushoto Musa Siwiti, ilimkuta Hasani na kuukwamisha mpira wavuni. Hadi tunaenda mapumziko Vijana wa Kibangu walikuwa wanaongoza kwa goli 3-1. Mwalimu wa timu ya Survey Veteran aliwasifia wachezaji wake kwa kujituma kwa nguvu zao zote katika kuhakikisha timu inapambana hadi mwisho.
"Japo tumefungwa ila tumeonesha kandanda safi lenye ushindani japo tulikuwa tunacheza na vijana" Hao yakuwa maneno ya Mwl R. Bomba.

0 comments:

Post a Comment