Tuesday, 22 December 2015

GASABILE VETERANS YAKIONA CHA MOTO KWA SURVEY VETERANS


Timu ya SVSC ilitoa kipigo kikali mbele ya Gasabile Veterans katika uwanja wao kwa kuibugiza magoli 4-1. SVSC ikicheza katika ubora wake, iliwachukua dakika 15 kupata goli la kuongoza kupitia beki wake hatari mwenye misuri minene na mashuti makali Ahmed Salumu baada ya kuwapita mabeki wa Gasabile na kuachia shuti kali la guu la Dhahabu na kuipatia SVSC goli la kuongoza. baadae Gasabile walisawazisha na hadi timu zinaenda mapumziko mabao yalikuwa 1-1.

Kipindi cha pili kilianza kwa kila timu kufanya mabadiliko na baadae kidogo timu ya SVSC ilipata magoli mawili ya haraka haraka kupitia fowadi wao hatari Dulla. Goli la nne liliwekwa kimiani kiufundi na winga hatari ambaye alikuwa katika kiwango bora katika mechi hiyo Musa Siwiti baada ya kuunganisha krosi safi iliyopigwa na beki mahili Ahmad Shaweji. Hadi mwisho wa mchezo SVSC walishinda kwa goli 4-1


0 comments:

Post a Comment