Sunday, 13 December 2015

TIMU YA VIJANA YA UKAGUZI YAIFUNGA SURVEY VETERANS GOLI 5-1


Timu ya vijana ya Ukaguzi imeifunga Survey Veterans goli 5-1 katika uwanja wake wa nyumbani katika mchezo uliochezwa jumapili tarehe 12/12/2015. Timu ya Vijana ya Ukaguzi ikichezesha Vijana wengi tofauti na Survey Veterans, iliwachukua dk 20 kupata magoli ma nne.Hii inatokana na uwezo wao kama vijana ukilinganisha na wazee wa Survey Veterans.Hadi timu zinaenda mapumziko, Timu ya vijana ya Ukaguzi ilikuwa inaongoza kwa goli 4-0.

Kipindi cha pili kilianza kwa kila timu kufanya mabadiliko na kila timu kupata goli moja moja. Hadi mwisho wa mchezo Timu ya Ukaguzi ilishinda goli 5-1.

0 comments:

Post a Comment